Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

13 DESEMBA 2022

13 DESEMBA 2022

Pakua

Jaridani leo tunakuletea mada kwa kina tukimulika mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu mkataba wa kimataifa wa bayoanuai CBD unaoendelea mjini Montreal Canada. Pia tunakuletea habari kwa ufupi kutoka huko huko Montreal Canada, nchini Somalia na nchini Haiti. Mashinani tunakuletea ujumbe wa mwanauchumi mashuhuri duniani Sir Partha Dasgupta, anasemaje?

  1. Hii leo huko Montreal Canada kunakoendelea mkutano wa 15 wa nchi wanachama wa mkataba wa kimataifa wa bayonuai, CBD, COP15, Umoja wa Mataifa umetambua harakati 10 zinazoendelea maeneo mbalimbali kwa ajili ya kurejesha mazingira asilia duniani na miongoni mwao ni Ukuta Mkubwa wa Kijani ambao ni mkakati wa kupanda miti kuanzia Afrika Magharibi nchini Senegal hadi Eritrea mashariki mwa Afrika ikiwa ni umbali wa zaidi ya kilometa 8000. 
  2. Uchunguzi wa hivi karibuni wa hali ya chakula nchini Somalia umeonesha kuwa hali bado si nzuri lakini haiwezi kufikia kiwango cha kutangaza kuweko kwa baa la njaa nchini humo kama ilivyokuwa inatarajiwa awali, ni kwa mujibu wa msemaji wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya dharura, OCHA Jens Learke akizungumza hii leo huko Geneva, Uswisi na waandishi wa habari
  3. Na hii leo shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, kanda ya Amerika, PAHO limesema Haiti imepokea dozi milioni 1.17 za chanjo dhidi ya kipindupindu kwa ajili ya kampeni ya chanjo inayotarajiwa kuanza siku chache zijazo kuupambana na ugonjwa huo ambao bado ni tishio nchini humo.  
  4. Na katika mashinani, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Mazingira duniani, UNEP limemtangaza mwanauchumi mashuhuri duniani Sir Partha Dasgupta kuwa bingwa wa mwaka huu 2022 wa shirika hilo katika kipengele cha Sayansi na ubunifu kutokana na kazi zake nzuri za kihistoria zinazohusisha uchumi wa bayoanuwai na maendeleo ya wananchi. Na hapa Sir Dasgupta anatoa ushauri kwa wachumi.

Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, Karibu!

Audio Credit
Anold Kayanda
Audio Duration
11'18"