Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

02 DESEMBA 2022

02 DESEMBA 2022

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazia ripoti ya WHO, habari kutoka Rwanda, makala inayomulika harakati za Umoja wa Mataifa za kusaidia wakulima wenye ulemavu na mashinani tunakwenda nchini Burkina Faso.

  1. Shirika la Umoja wa Matifa la afya ulimwenguni WHO leo limezindua ripoti ya mwongozo mpya wa, “Nini kinachofanya kazi ili kuzuia ukatili dhidi ya Watoto mtandaoni”, ripoti ambayo inatoa njia za kushughulikia wasiwasi unaoongezeka duniani kote wa kuwaweka watoto salama mtandaoni, kwa kuzingatia aina mbili za ukatili mtandaoni.    
  2. Kuelekea siku ya kimataifa ya watu wenye ulemavu duniani kesho tarehe 3 mwezi Desemba, maudhui makuu yakiwa nafasi ya uvumbuzi katika kuchochea dunia yenye fursa za kufikiwa na zenye usawa kwa wote, tunakwenda nchini Rwanda ambako huko mashindano ya ulimbwende kwa mwaka huu wa 2022 yalikuwa ya aina yake kwani kwa mara ya kwanza mshiriki ambaye ni bubu na kiziwi alijumuika na kuibuka mshindi wa kipengele cha uvumbuzi. 
  3. Makala inamulika harakati za Umoja wa Mataifa za kuhakikisha wakulima wenye ulemavu nao wanaweza kujipatia kipato kama wakulima wengine ili hatimaye kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, ikiwemo la kutokomeza umaskini. Msimulizi wetu katika makala hii iliyoandaliwa na mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya kilimo, IFAD
  4. Na katika mashinani wakati leo dunia ikiadhimisha siku ya Kimataifa ya Kukomesha Utumwa, na aina moja yapo ya utumwa huo unaotajwa ni ajira za utotoni tunakupeleka nchini Burkina Faso. Mtoto Domboué Nibéissé akiwa na umri wa miaka tisa aliacha kwenda shule na badala yake kutumikishwa kwenye mashamba ya pamba.

Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

Audio Duration
11'42"