Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

06 DESEMBA 2022

06 DESEMBA 2022

Pakua

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina na tukiwa tungali katika siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na wasichana duniani, tunamulika wale wanaowapokea manusura wa ukatili wa kijinsia nchini Kenya. Pia tunakuletea habari kwa ufupi na mashinani kutoka Uganda.

  1. Mkurugenzi mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa mazingira UNEP  ameonya kwamba “Tuko katika vita na asili na ni lazima kurejesha amani na asili kwa ajili ya mustakbali bora wa sayari dunia na viumbe vtyote vilivyopo.” Inger Andersen ametoa onyo hilo wakati viongozi wa dunia wakikutana Montereal Canada kwenye mkutano wa Umoja wa Mastaifa wa bayoanuai CBD wa COP15 ili kukubaliana kulinda bayoanuai ya dunia.   
  2. Zaidi ya raia 80,000 wa Somalia wamewasilia katika kambi ya wakimbizi ya Daadab nchini Kenya, katika kipindi cha miaka miwili iliyopita wakikimbia ukosefu wa usalama na ukame nchini mwao, na kati yao hao 24,000 wamewasili tangu mwishoni mwa mwezi Septemba mwaka huu, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi duniani, UNHCR.
  3.  Na Kamati ya Umoja wa Mataifa ya biashara na maendeleo UNCTAD imesema lazima kuwepo kwa ufumbuzi kuhusu mgogoro wa madeni wakati kukiwa na hali mbaya ya migogoro na ukosefu wa usawa na nchi zinazoendelea zikikabiliwa na ongezeko la hatari za mzigo mkubwa wa madeni.  
  4. Katika mashinani tukiwa bado katika siku 16 za kuhamasisha mapambano dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake na wasichana tutaelekee nchini Uganda. Msanii Mwanamuziki Sheebah Karungi ana maoni gani?

Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
12'13"