Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

05 DESEMBA 2022

05 DESEMBA 2022

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazia udongo na Ukraine. Pia tunakuletea makala ya wakimbizi wa Burundi na mashinani tutaangalia mafunzo waliyopatiwa wabunge nchini Sudan Kusini.

  1. Ikiwa leo ni siku ya udongo duniani , shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO limesisitiza umuhimu wa kuhifadhi udongo ili kuhakikisha unaendelea kuleta tija kwa maisha ya mamilioni ya watu duniani wanaotegemea chakula  kutoka kwenye kilimo kwani  udongoni ndiko chakula kinakoanzia.. 
  2. Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu Volker Türk ameanza ziara ya siku nne nchini Ukraine hapo jana Jumapili Desemba 4 kwa mwaliko wa Serikali ya nchi hiyo akiwa ameongozana na wafanyakazi wa ofisi yake wanaohusika na kufuatilia masuala ya haki za binadamu..   
  3. Makala tunasimulia safari ya wakimbizi wa Burundi waliorejea nyumbani kutoka Tanzania na wito wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR kwa jamii ya kimataifa.  
  4. Na katika mashinani, Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS kwa ushirikiano na Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa marendeleo, UNDP umeendesha mafunzo kwa wabunge wapya nchini Sudan Kusini kuhusu kuimarisha usimamizi wa kupambana na rushwa. Claudia Sayago ni Afisa Mwandamizi wa Masuala ya Mahakama, Utawala wa Sheria wa UNMISS, anasemaje?

Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
11'50"