Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

15 DESEMBA 2022

15 DESEMBA 2022

Pakua

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina tukimulika ukuaji wa lugha ya Kiswahili nchini Rwanda. Na habari kwa ufupi kutoka nchini Thailand, Ukraine na DR Congo. Katika kujifunza lugha ya Kiswahili Dkt. Josephat Gitonga atafafanua maana ya methali “Usishindane na kari, kari ni mja wa Mungu”.

  1. Katika mkutano wa kimataifa kuhusu Ukimwi unaoendelea huko Thailand, washiriki wamepitisha makubaliano ya kutambua nafasi kubwa ya jamii katika kukabili janga la UKIMWI wakisema hatua zinazoongozwa na jamii ziwe rasmi au si rasmi ni lazima zipewe kipaumbele kwenye ufadhili.
  2. Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya  kuratibu misaada ya dharura, OCHA, Martin Griffiths ametamatisha ziara yake ya siku nne nchini Ukraine na kutaja mambo makuu matatu muhimu ya kupatiwa kipaumbele kuwa ni mosi; kurejesha umeme kwenye makazi, pili kutegua mabomu yaliyoko kwenye makazi ya watu na tatu, ni kuchechemua shughuli za kiuchumi ili maisha yaweze kuendelea na kwamba Umoja wa Mataifa uko tayari kusaidia.  
  3. John Bosco Ntaganda, kiongozi wa zamani wa waasi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo aliyehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC mwezi Novemba mwaka 2019 baada ya kupatikana na hatia ya makosa 18 ya uhalifu wa kivita na uhalifu wa kibinadamu huko Ituri jimboni, DRC amewasili nchini Ubelgiji tayari kuanza kutekeleza adhabu yake kwenye gereza la Leuze-en-Hainaut nchini humo
  4. Na katika kujifunza Kiswahili Dkt. Josephat Gitonga atafafanua maana ya methali “USISHINDANE NA KARI, KARI NI MJA WA MUNGU”.

Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, Karibu!

Audio Credit
Anold Kayanda
Audio Duration
12'36"