08 Januari 2021
Leo ni Ijumaa na tunakuletea mada kwa kina na tunaangazia maonesho ya sanaa ya uchoraji picha yaliyofanywa jijini Nairobi Kenya na Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na madawa na uhalifu, UNODC. Picha hizo zimechorwa na watoto walioko chini ya uangalizi maalum wa kubadili tabia zao baada ya kukutwa na hatia za makosa mbalimbali nchini Kenya. Halikadhalika tunabisha hodi nchini Tanzania katika Baraza la Kiswahili la Taifa, BAKITA kupata maana za maneno MCHAPO bila kusahau Habari kwa Ufupi ikimulika habari muhimu kwa siku ya leo. Mwenyeji wako ni Flora Nducha! karibu.