Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

04 JANUARI 2021

04 JANUARI 2021

Pakua

Katika Jarida la Habari za umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea

-Watu zaidi ya 100 wauawa katika shambulio kwenye jimbo la Tillaberi nchini Niger, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alaani vikali shambulio hilo na kutaka wahusika wakamatwe na kuwajibishwa.

-Nchini Pakistan wachimba migodi ya makaa ya mawe 11 wameuawa katika shambulio la kigaidi lililotokea mwishoni mwa wiki kwenye jimbo la Balouchistan, watu wengine wengi wamejerihiwa na wengine kutekwa .

-Leo ni siku ya nukta nundu duniani ambayo kila mwaka huadhimishwa Januari 4. Umoja wa Mataifa umesema ni muhimu kuhakikishataarifa zinamfikia kila mtu ikiwemo wanaotumia maandishi ya nukta nudu ili waasiachwe nyuma

-Mada yetu kwa kila inamulika siku hii ya nukta nudu na utamsikia mmoja wa watu wenye ulemavu wa kutoona na anayetumia maandishi ya nukta nundu

-Na mashinani leo tunakwenda Kenya ambako shule nyingi zimefunguliwa leo na UNICEF iko katika kampeni kubwa ya kuwahamasisha wazazi kuwarejesha shuleni watoto baada ya shule kufungwa kwa muda mrefu kutokana na janga la COVID-19

Audio Credit
UN News/ Flora Nducha
Audio Duration
10'6"