Katika Jarida la Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea
- Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa atoa wito wa kuhakikisha mizozo inasitishwa na mizizi yake kukatwa kwa lengo la kudumisha amani na kufikia ajenda ya maendeleo ya 2030 hususan brani Afrika.
-Walinda amani kutoka Burundi, Bangladesh na Cameroon waliopoteza maisha Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR wakati wa Krisimasi waagwa na kusafirishwa makwao kwa maziko
-Kutana na Libaree Muyumba kiutoka Rwanda mnufaika wa msaada wa chakula wa WFP ambaye sasa anafanyakazi na shirika hilo kusaidia wakimbizi wa Burundi kambini Mahama
-Maskala yetu leo inammulika kijana mjasiriamali kutoka Kenya anayesema fikra za kuajiriwa baada ya masomo huwaponza vijana wengi wasiendelee
-Na mashinani utapata ujumbe kutoka kwa mkuu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO kuhusu vita vinavyoendelea dhidi ya janga la corona au COVID-19