Mjumbe wa amani wa UM Leonardo DiCaprio ashinda tuzo ya Oscar
Mcheza filamu nyota wa Marekani na mjumbe wa amani wa Umoja wa Mataifa Leonardo DiCaprio ni miongoni mwa washindi wakubwa katika tuzo za Academy mjini Hollywood zilizotolewa Jumapili usiku.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 41 ambaye labda anajulikana sana kwa kushiriki filamu ya 'Titanic, amejishindia Oscar ya kuwa mwigizaji bora kutokana na ushiriki wake katika filamu ya 'The Revenant.'