Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari kwa Ujumla

UN/Michael Ali

DRC: Asante MONUSCO kwa kuniepusha kuwa mpiganaji msituni

Bila MONUSCO ningalikuwa bado msituni – Mpiganaji wa zamani DRC

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kazi ya kuhesabu kura za Rais kufuatia uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 20 na kuendelea katika maeneo mengine siku zilizofuata, inaendelea huku nao wanufaka wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO ambao umeanza kufunga virago, wakitoa shukrani zao. Ufafanuzi zaidi anakupataia Anold Kayanda.

Sauti
1'31"

27 DESEMBA 2023

Hii leo jarida linajikita barani Afrika likianzia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kuangazia uchaguzi, wapiganaji wa zamani na MONUSCO, halikdhalika Jiko Point na mashinani ni nchini Kenya.

Sauti
9'57"
MONUSCO/Force

Baada ya mashambulizi kutoka CODECO maisha yarejea hali ya kawaida huko Fataki, Ituri

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kazi ya kuhesabu kura inaendelea baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika Jumatano na kuendelea katika baadhi ya maeneo jana Alhamisi, huku ikielezwa kwamba jimboni Ituri, maisha  yamerejea katika hali ya kawaida kwenye eneo la Fataki baada ya mwaka mmoja wa mashambulizi kutoka kwa wanamgambo waliojihami wa kundi la CODECO. 

Sauti
1'20"
©UNDP/Julie Pudlowski

UN: Siku ya Kimataifa ya Mshikamano wa Binadamu ni kusherehekea Umoja wetu katika tofauti zetu

DAFI, Mfuko wa Ufadhili wa Kimasomo kwa Wakimbizi, kwa kushirikiana na UNHCR wanawasaidia wakimbizi kutimiza ndoto zao za kupata elimu ya juu katika nchi ya kwanza wanakopata hifadhi baada ya kuzikimbia nchi zao. 

Idadi ya waliokwisha kunufaika na ufadhili wa DAFI inazidi kuongezeka lakini takwimu za hivi karibuni zinaonesha angalau hadi kufikia mwaka jana 2022 DAFI ilipotimiza miaka 30 tangu kuanziswa kwake, chini ya serikali ya Ujerumani na wadau wengine, tayari imewafadhili wakimbizi zaidi ya 24,000 kusoma elimu za juu iwe vyuo vikuu au vyuo vingine vya ujuzi.

Sauti
3'22"
© UNICEF

UNICEF Tanzania: Chanjo ya polio sio tu inamlinda mtoto bali inaokoa maisha

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linahimiza kila nchi kuhakikisha watoto wote wenye umri wa chini ya miaka 5 wanapatiwa chanjo dhidi ya polio ugonjwa ambao sio tu unasababisha ulemavu kwa watoto lakini pia ukakatili maisha yao. Kwa msaada kutoka wakfu wa Bill na Melinda gates hivi karibuni UNICEF na shirika la afya duniani WHO nchini Tanzania walizindua kampeni kubwa ya chanjo dhidi ya ugonjwa huo iliyowafikia watoto zaidi ya milioni 4. 

Sauti
2'17"