Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari kwa Ujumla

Lugha ya Kiswahili yazidi kuenea kwenye medani za kimataifa

Kwa mara ya kwanza ripoti ya Maendeleo ya binadamu inayoandaliaw na shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa imekuwa na muhtasari wake katika lugha ya Kiswahili. Uzinduzi wa muhtasari huo ulifanyika Kilifi, Mombasa Kenya tarehe 12 mwezi huu wa Juni na siku ya Alhamisi ya tarehe 20 Juni mjini New York Marekani, ubalozi wa Kenya ukafanya uwasilishaji wa muhtasari huo. Je nini kilijiri? Ungana na Assumpta Massoi katika makala hii ya wiki.

STUDIO: ASSUMPTA pckg

Miaka 50 ya Umoja wa Afrika umeshuhudia mafanikio: Ban

Umoja wa Mataifa unajivunia kuendelea kushirikiana na Umoja wa Afrika na wakazi wa bara hilo katika kuweka mazingira ya fursa na matumaini kwa wote, ni ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon hii leo tarehe 25 Mei, ambapo Umoja wa Afrika uliotokana na Umoja wa nchi huru za Afrika, OAU unatimiza miaka 50 tangu kuanzishwa kwake.  Amesema wakati waafrika wanakumbuka waasisi na magwiji wa karne ya 20 waliojitolea kwa hali na mali kupigania ukombozi na Umoja, ni wakati muhimu pia kuwa na matarajio ya zama za ustawi na amani.

Athari za teknohama zaangaziwa Geneva

Wakati dunia itaadhimisha siku ya kimataifa ya Jamii habari tarehe 17 mwezi huu, wawakilishi wa nchi wanachama wa Taasisi ya kimataifa ya mawasiliano ITU, taasisi za kimataifa, na wawakilishi wa Umoja wa Mataifa wanamkutana mjini Geneva, Uswisi, katika mkutano wa siku tatu unaolenga kuchukua mrejesho wa  lengo lililowekwa na wanachama hao la kuhakikisha dunia inafaidika na Jamii Habari ifikapo mwaka 2015. Mkutano huo ambao pia utaangazia athari za matumizi mabaya ya teknolojia ya habari na mawasiliano , Teknohama, na namna ya kuzikabili, utatumia miongozo iliyotolewa kwa kila nchi ili kutim

Zebaki ni tishio kwa afya ya binadamu

Madini ya zebaki yana umuhimu mkubwa kwa maisha ya kila siku ya mwanadamu, lakini madini haya pia yametajwa kuwa na athari nyingi za afya ya mwanadamu kwa miaka mingi pasipo wengi kufahamu athari zake.

Utafiti unaonyesha kuwa viwango vya zebaki duniani vinaendelea kuongezeka vikichochewa kila siku za shughuli za mwanadamu zikiwemo uchomaji wa makaa ya moto na uchimbaji wa madini ya dhahabu. Zebaki huingia majini na kisha kuingia kwenye mwili wa binadamu kupitia ulaji wa samaki waliovuliwa kwenye maji hayo yenye madini ya Zebaki.