Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari kwa Ujumla

WFP/Hugh Rutherford

FAO Tanzania yawasaidia wakulima kurutubisha lishe kupambana na utapiamlo

Nchini Tanzania shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) kwa kushirikiana na serikali na wadau wake wameandaa mpango wa miaka mitano wenye lengo la kuoanisha shughuli za kilimo na lishe ili kukabiliana na utapiamlo. Devota Songorwa wa Radio washirika KidsTime FM ametuandalia taarifa hii kutoka Dodoma nchini Tanzania.

(TAARIFA YA DEVOTHA SONGORWA)

Sauti
2'12"
© UNICEF/Helene Sandbu Ryeng

UNICEF yawasaidia maelfu ya watoto masikini Kenya kusomea nyumbani

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF , nchini Kenya, limegawa redio 10,000 zinazotumia nishati ya sola kwa kaya masikini nchini humo ili watoto wengi wapate fursa ya kusoma nyumbani wakati huu wakijianda kurejea shuleni. Tupate maelezo zaidi na Jason Nyakundi 

(TAARIFA YA JASON NYAKUNDI) 

Katika eneo la mtaa wa mabanda la Kibera jijini Nairobi 

 …Natts…  

Sauti
2'35"
©FAO/Kenya Team

FAO yawapiga jeki wafugaji na wakulima Togo

Maji ni hai ni kauli ambayo imethibitika kwa wakazi wa jimbo la Dankpen nchini Togo, baada ya Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la chakula na kilimo, FAO na serikali, kukarabati bwawa linalotumika hivi sasa kwa shughuli siyo tu za umwagiliaji, bali pia maji kwa wanyama na utalii. Jason Nyakundi na taarifa zaidi

(TAARIFA YA JASON NYAKUNDI)

Bustani ya mboga imeshamiri katika mkoa wa Dankpen nchini Togo, umwagiliaji ukiendelea, na maji yakichotwa kutoka bwawa la Gbangbale lililokarabatiwa na FAO.

Sauti
1'55"
UN News/ John Kibego

IFAD yasaidia maendeleo ya kilimo Senegal

Nchini Senegal, wakulima na wafanyabiashara wadogo wameushukuru mradi wa kusaidia maendeleo ya sekta ya kilimo, PAFA, unaofadhiliwa na Mfuko wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo IFAD. Anold Kayanda na maelezo zaidi. 

(TAARIFA YA ANOLD KAYANDA)

Katika eneo la Niakhar, mkoa wa Fatick nchini Senegal, shughuli za kuvuna mtama zinaendelea kwenye mashamba yanayomilikiwa na chama kijami cha michezo na utamaduni cha Jamm Bugum.  

Sauti
1'30"
© UNFPA/Lauren Anders Brown

Wanawake wametaabika sana mwaka 2020:UNFPA

Mwaka 2020 ukielekea ukingoni, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya idadi ya watu, UNFPA, Dkt. Natalia Kanem amesema mwaka huu wa 2020 ulikuwa ni mwaka wa janga kuu zaidi kwa wanawake na wasichana ambao tayari walikuwa kwenye masahibu hata kabla ya janga hilo. Kulikoni? Assumpta Massoi na taarifa zaidi

(TAARIFA YA ASSUMPTA MASSOI)

Mwaka 2020, mwaka tofauti na miaka mingine kabisa!

Ndivyo anavyoanza ujumbe wake Dkt. Natalia Kanem, Mkuu wa UNFPA akitoa tathmini ya mwaka 2020 .

Sauti
1'45"
UN photo / Catianne Tijerina

Kuelekea uchaguzi mkuu CAR, mwamko mkubwa kwa wananchi wa CAR waonekana.

Wapiga kura nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, wameanza kuchukua kadi zao za mpiga kura tayari kwa ajili ya uchaguzi mkuu utakaofanyika jumapili hii ya tarehe 27 mwezi Desemba. 

Nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, harakati zikiendelea mitaani huku katika vituo vya kujiandikishia, wananchi waliojiandikisha kupiga kura kwa uchaguzi mkuu jumapili wakichukua vitambulisho vyao.

Ari ni kubwa ili kumaliza mgawanyo na ghasia uliogubika taifa hilo tangu mwaka 2013.

Sauti
2'7"
UNICEF Malawi Video capture

Kuteka maji mbali kulinikwamisha kwenye hesabu lakini UNICEF imenikomboa- Elina

Nchini Malawi mradi wa kusukuma maji kwa kutumia nishati ya jua au sola uliowezeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF umekuwa mkombozi kwa wanafunzi na jamii zinazozunguka mradi huo uliojengwa katika mkoa wa kati. John Kibego na maelezo zaidi.

Katika mkoa wa kati wilaya ya Dedza nchini Malawi, ukame umekuwa chanzo cha ukosefu wa maji iwe shuleni au nyumbani.

Elina Chikumbutso mwanafunzi mwenye umri wa miaka 15 anasema anapenda hesabu lakini uhaba wa maji umesababisha atumie muda mrefu kusaka maji na hivyo kuchelewa darasani kujifunza.

Sauti
1'54"
© UNICEF

Walinivua nguo wakanivuta sehemu zangu, mtoto aeleza. UNICEF yaingilia kati.

Nchini Kenya, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, kwa msaada wa shirika la Uingereza, UK Aid, linasaidia kutoa huduma ya ulinzi kwa watoto katika makazi  duni au yasiyo rasmi, Korogocho, walioathiriwa na kufungwa kwa shule kutokana na janga la COVID-19. Jason Nyakundu anaeleza zaidi.

Korogocho, Kenya, eneo la makazi duni lenye ukubwa wa kilomita moja na nusu za mraba na idadi ya watu inayokadiriwa kufikia laki mbili. 

Sauti
2'35"
UNMISS\Nektarios Markogiannis

Mkazi wa Sudan Kusini: Sioni sababu ya mtoto wa kike kuwa na thamani zaidi kuliko ng'ombe

Nchini Sudan Kusini, wakazi wa jimboni Bahr-el-Ghazal wameelimishwa jinsi ya kuripoti matukio ya ukatili wa kingono na unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake, tukio ambalo limechagizwa na ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo. John Kibego na taarifa kamili.

Ndani ya moja ya studio za redio ya jamii jimboni Bahr-el-Ghazal, kaskazini-magharibi mwa Sudan Kusini washiriki wanajadili harakati za kukabili ukatili wa kijinsia. Miongoni mwao ni Maria Angelo mkazi wa Aweil akieleza jukumu lao. 

Sauti
2'5"