Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ziara ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Barani Afrika!

Ziara ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Barani Afrika!

Pakua

Wiki hii Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amezuru barani Afrika akianzia Ukanda wa Maziwa Makuu ambapo ametembelea Burundi na Jamhuri  ya Kidemokrasia ya congo DRC na hatimaye akaelekea Sudan Kusini ambako kwenye nchi hizo tatu amemulika umuhimu wa kukuza amani na demokrasia kupitia mazungumzo jumuishi ya kisiasa.

Lengo la ziara yake pia lilikuwa ni kumulika umuhimu wa usaidizi wa kibinadamu wakati ambapo Umoja wa Mataifa unatarajia kuandaa Kongamano la Kimataifa kuhusu maswala ya kibinadamu litakalofanyika mjini Istanbul nchini Uturuki, Mwezi Mei Mwaka huu.  Basi kwa kile kilichojiri katika ziara hiyo tuungane na Priscilla Lecomte.

Photo Credit
Katibu MKuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.(Picha:UM/Eskinder/Debebe)