Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari kwa Ujumla

Pamoja na ARV's lishe na ushauri nasaha ni muhimu kwa wagonjwa wa ukimwi

Wakati ripoti ya shirikika la Umoja wa Mataifa la kupambana na HIV na ukimwi UNAIDS iliyotolewa leo imesema ingawa maambukizi mapya yamepungua na vifo vitokanavyo na ukimwi vimepungua lakini matunzo kwa waathirika la lishe ni muhimu sana katika kuokoa maisha ya wagonjwa.

Mwandishi wa kujitegemea Osca Mashanga akiwa Nairobi, Kenya amefuatilia kuhusu juhudi za vituo vya afya kuelimisha, kusaidia na kutoa mafunzo na ushauri kwa wagonjwa wa ukimwi ili kusaidia kuboresha afya zao. Msikilize

(MAKALA NA OSCAR MASHANGA)

Juhudi za kupambana na upofu nchini Kenya

 

Makala yetu ya wiki hii inaangazia siku ya kuona duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka alhamisi ya pili ya mwezi Oktoba. Shirika la afya duniani WHO limesema katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya kuona kwamba mkazo wa kimataifa unapaswa kuelekezwa katika kupunguza upofu, matatizo ya kutoona mbali au karibu na kuwasaidia wasioona.

Usambazaji chakula wa WFP nchini Libya washika kasi

Zaidi ya watu 20,000 wengine walioukimbia mji huo wanatarajiwa kupokea chakula hicho siku chache zijazo. WFP kwa ushirikiano na shirika la mwezi mwekundu pia watagawa chakula kwa watu 85,000 kwa muda wa wiki mbili zijazo kwenye mji wa Benghazi na maeneo yaliyo karibu.

Hao ni watu ambao mara nyingi wanategemea chakula kinachosambazwa kupitia kwa mfumo wa serikai jinsi anavyoeleza Emilia Casella kutoka WFP.

(SAUTI YA EMILIA CASELLA)

UM watupilia mbali kesi ya Georgia mahakama ya ICJ

Mahakama hiyo ya ICJ iliyo Hague inasema kuwa haitashughulikia kesi hiyo kwa kuwa majadiliano ya kutafuta suluhu hayakuwa yamefanyika kati ya pande husika. Georgia ilidai kuwa Urusi na waasi hao waliendesha ghasia za kikabila dhidi ya raia wa Georgia kwenye maeneo ya Abkhazia na Ossetia kusini.

Urusi ilichukua udhibiti wa maeneo hayo mawili mwaka 2008 na kusababisha maelfu ya raia wa Georgia kuyakimbia maeneo hayo na ambao hadi sasa ni wakimbizi wa ndani nchini Georgia.