Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari kwa Ujumla

John Kibego

UNICEF yawatumia viongozi wa dingi kuhamasisha kampeni ya chanjo ya COVID-19 Garissa

Janga la ugonjwa wa Corona au COVID-19 likiendelea kutikisa dunia huku taarifa potofu kuhusu chanjo zikiendelea kusambaa, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini Kenya limechukua hatua ya kushirikiana na viongozi wa dini ikiwemo wale wa madhehebu ya kiislamu ili kusaidia kuelimisha waumini wao juu ya chanjo na faida zake katika kuepusha kusambaa zaidi kwa virusi vinavyosababisha ugonjwa huo. Taarifa ya John Kibego inafafanua zaidi.
(Taarifa ya John Kibego)
Nats..

Sauti
2'12"
UNFPA

Hakimiliki ya mwili mtandaoni ni muhimu sana kwa wanawake:UNFPA

Kampeni mpya iliyozinduliwa mwezi huu wa DFesemba na shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu duniani linalohusika pia na afya ya uzazi UNFPA ya “Hakimiliki ya miwli wa binadamu” ina lengo la kuwasukuma watunga sera, sekta za teknolojia na mitandao yote ya kijamii kuuchukulia unyanyasaji na ukatili wa miili ya binadamu hususani ya wanawake mtandaoni kuwa ni suala linalohitaji kupewa uzito kama ilivyo ukiukwaji wa hakimiliki zingine. Flora Nducha na taarifa kamili 
(TAARIFA YA FLORA NDUCHA) 

Sauti
2'3"
© UNICEF/Karel Prinsloo

Mabadiliko ya tabianchi yawaathiri wafugaji Arusha Tanzania

Umoja wa Mataifa ukiendelea kutaka hatua zaidi kwa ajili ya tabianchi kama njia mojawapo ya kukabiliana na madhara ya mabadiliko ya tabianchi nchini Tanzania madhara hayo yako dhahiri kwa wafugaji wa wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha ambao kupitia taarifa hii iliyoandaliwa na Mathias Tooko wa Radio washirika Loliondo FM wanaeleza hali ilivyokuwa zamani na sasa.
(Taarifa ya Mathias Tooko)

Sauti
1'54"
UNMVC

Majaribu yatakabili dunia lakini tuazimie kuondokana nayo- Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametuma salamu za mwaka mpya wa 2022 akitaka dunia iazimie kwa pamoja mwaka huu mpya uwe wa kuondokana na majaribu yanayotarajia kuikumba.

Katika ujumbe wake kwa njia ya video Guterres ametaja majaribu hayo kuwa ni  ongezeko la umaskini na ukosefu wa usawa, mgao wa chanjo za COVID-19 usio na uwiano, ahadi za tabianchi zenye pengo, ongezeko la mizozo, migawanyiko na taarifa potofu.

Sauti
1'57"
MINUSCA/Leonel Grothe

Tunatuma salamu za sikukuu kwa raia wa CAR na tunawatakia mwaka mpya wenye amani - TANBAT 5

Katika kuelekea kuukamilisha mwaka 2021 na kuingia katika mwaka mpya wa 2022, Walinda amani wa Kikosi cha 5 cha Tanzania kinacholinda amani nchini Jamhuri ya  Afrika ya Kati, CAR, TANBAT 5 wametuma salamu za kuwatakia msimu wa sikukuu za Krismasi na mwisho wa mwaka raia wanaowalinda. Kupitia taarifa hii iliyoandaliwa na Kapteni Asia Hussein ambaye ni Afisa Habari wa kikosi hicho, anayeanza kutuma salamu ni Luteni Philipo Denis Msaki anayesimamia ukuzaji uhusiano kati ya vikosi, jamii pamoja na asasi za kiraia.

Sauti
2'17"
© FAO Cameroon

Sophie afurahia mradi wa UNHCR ulivyomnusuru kiuchumi ukimbizini

Nchini Cote d’Ivoire  shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limeleta tabasamu na nuru kwa wakimbizi ambao biashara zao zilivurugika kutokana na janga la ugonjwa wa Corona au COVID-19 ambalo limetikisa dunia kuanzia mwaka jana wa 2020. Kwa sasa wakimbizi hao wakiwemo wa kutoka Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC wana imani ya kujiinua tena kiuchumi kama anavyosimulia Happiness Pallangyo wa Radio washirika Radio Uhai FM ya Tabora Tanzania katika taarifa hii iliyoandaliwa na UNHCR.

Sauti
2'39"
FAO Tanzania

FAO yajivunia ushirikishaji vijana kwenye kilimo

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo, FAO Qu Dongyu ametoa ujumbe wake kwa mwaka mpya wa 2022 huku akitaja mafanikio ambayo shirika hilo limefanikisha mwaka huu wa 2021 licha ya changamoto ya janga la ugonjwa wa Corona au COVID-19.
Katika salamu hizo kwa njia ya video Bwana Qu amesema mafanikio hayo ni pamoja na mikutano waliyoendesha ili kufanya kazi usiku na mchana kuleta mabadiliko yanayoweza kuondoa njaa duniani.

Sauti
1'47"
UN Women Tanzania/Deepika Nath

Barua mahsusi ya watoto kwa Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF ambalo limetimiza miaka 75 mwezi huu, kwa miaka yote hiyo tangu mwaka 1946 limekuwa likitoa msaada kwa watoto kote ulimwenguni wakiwemo watoto wa Tanzania. Katika kuadhimisha kumbukumbu hii ya miaka 75, watoto kadhaa wa Tanzania wamemwandikia barua Rais wao, Samia Suluhu Hassan kuzungumzia changamoto zinazowakabili. Kwa ajili ya uwakilishi tu, barua hiyo inasomwa na mtoto Tumaini George akisaidiwa na Mwanaharakati wa masuala ya vijana Meena Ally, pamoja na mshairi maarufu nchini humo, Mrisho Mpoto.

Sauti
2'33"
© World Bank/Arne Hoel

Mkimbizi arejea nyumbani na kufuga kuku sasa ni mfano kwa wenzake Burundi

Kijana Evariste Niyonzima mkazi wa sasa wa viunga vya jiji la Bujumbura nchini Burundi aliporejea nchini mwake kutoka ukimbizini katika nchi jirani ya Tanzania, alikuwa na mawazo kuwa atakapomaliza tu masomo atapata ajira ya ofisini itakayompa kipato hadi pale alipogundua kuwa hali halisi ni tofauti na alivyofikiria. Hata hivyo hivi sasa amefanikiwa kuliko hata baadhi walioajiriwa ofisini. Alifanyaje? Edwije EMERUSENGE ni mwandishi wa Televisheni washirika, Mashariki TV ya Burundi ameipata siri ya mafaniko anasimulia zaidi.

Sauti
2'35"
MINUSMA/Harandane Dicko

Utani baina ya makabila ni moja ya mbinu za kuchagiza amani na maelewano

Tofauti zinapaswa kuimarisha jamii badala ya kuisambaratisha, huo ndio  ujumbe uliotamalaki wakati wa kampeni iliyoendeshwa nchini Mali na ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuweka utulivu nchini humo MINUSMA kwa kushirikiana na chama cha wadau wa Umoja wa Mataifa nchini humo, MANU. Kampeni ilileta pamoja wazee kwa vijana, wanawake kwa wanaume pamoja na Watoto wenye vipaji vya Sanaa na utamaduni. Nini kilifanyika, tujiunge na Jason Nyakundi katika taarifa hii.

Sauti
2'39"