Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban atiwa hofu na uchaguzi Comoro

Ban atiwa hofu na uchaguzi Comoro

Pakua

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  Ban Ki-moon amesema anafuatilia kwa wasiwasi maendeleo chini Comoro tangu tangazo la tume ya taifa ya uchaguzi CENI,  la matokeo ya awali ya uchaguzi wa Rais wa muungano wa nchi hiyo na awamu ya kwanza ya  uchaguzi wa magavana wa visiwa vya Comoro Kuu, Anjouan na Mohéli.

Taarifa ya msemaji wa Katibu Mkuu imesema kuwa Bwana Ban ameitaka serikali , wagombea, wadau wengine na taasisi husika katika mchakato wa uchaguzi, kujizuia dhidi ya machafuko na kuhakikisha sheria zinatumika.

Uchaguzi huo umefanyika Jumapili tarehe 21 mwezi wa Februari ambapo awamu ya pili itakayoshindanisha washindi wa awamu ya kwanza itafanyika  mwezi Aprili.

Kwa mujibu wa katiba ya nchi, kiti cha urais nchini Comoro kinazunguka katika visiwa hivyo vitatu ambapo awamu hii ni zamu ya Comoro Kuu

Photo Credit