Asante Katibu Mkuu kwa kuendelea kuniamini: Elizabeth Mrema
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres Jumanne wiki hii alimtangaza Elizabeth Maruma Mrema kutoka nchini Tanzania kuwa naibu mkurugenzi mtendaji mpya wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa mazingira UNEP.
Bi Mrema tangu mwaka 2020 amehudumu kama katibu mtendaji wa sekretarieti ya mkataba wa Umoja wa Mataifa wa bayoanuai CBD, yenye makao yake makuu mjini Montreal, Canada akizungumza na Idhaa hii ya Kiswahili baada ya uteuzi huo ameelezea alivyoupokea
(SAUTI YA ELIZABETH MREMA)