Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari kwa Ujumla

Ban Ki-moon alaani mauaji ya Sheikh Al-Nimr nchini Saudia

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, ameeleza kushtushwa sana na mauaji ya watu 47 nchini Saudi Arabia, akiwemo Sheikh Nimr Baqir Al-Nimr, kama ilivyotangazwa na Waziri wa Mambo ya Ndani Jumamosi hii.

Bwana Ban amesema hayo kwenye taarifa iliyotolewa na msemaji wake, akiongeza kwamba alikuwa amezungumzia kesi ya Sheikh Al-Nimr mara kadhaa na uongozi wa Saudia.

Sheikh An-Nimr na wafungwa wengine waliouawa tarehe pili Januari walihukumiwa kifo baada ya kesi iliyozua mashaka kuhusu usawa wake.

Martin Kobler atuma salamu za mwaka mpya kwa Walibya

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Libya Martin Kobler, ametuma salamu zake za mwaka mpya kwa raia wa Libya akiwatakia amani, matumaini na ukuaji wa uchumi.

Kwenye ujumbe wake uliotolewa tarehe mosi Januari, Bwana Kobler amesema ingawa mwaka wa 2015 haukuwa na baraka kwa Libya, makubaliano ya kisiasa yaliyosainiwa mwisho wa mwaka yameleta matumani, akiongeza kwamba mwaka 2016 utakuwa mwaka wenye fursa ya kukomesha mzozo wa Libya na kujenga upya amani na umoja wa nchi.

Ban Ki-moon apongeza Rais Museveni na Muungano wa Afrika kwa mazungumzo ya amani Burundi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekaribisha kuanzishwa upya kwa mazungumzo ya kisiasa baina ya pande kinzani za Burundi nchini Uganda.

Kwenye taarifa iliyotolewa na msemaji wake, Katibu Mkuu amepongeza jitihada za Rais wa Uganda Yoweri Museveni ambaye ni mpatanishi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa mazungumwo hayo.

Bwana Ban amezisihi pande za mzozo wa Burundi kushiriki kikamilifu kwenye mazungumzo hayo ili kukabili changamoto za kisiasa zinazoikumba nchi hiyo. Aidha amewaomba viongozi wa Burundi kuwajibika na kuipa kipaumbele amani na maridhiano.

Serikali zafikia makubaliano kuhusu mabadiliko ya tabianchi

Zaidi ya nchi 190 zimefikia makubaliano juu ya mazungumzo ya mabadiliko ya tabianchi.

Makubaliano hayo yamefikiwa baada ya siku saba ya mazungumzo nchini Uswisi, katika utaratibu wa maandalizi ya kongamano kubwa litakalofanyika mjini Paris, Disemba mwaka huu.

Christiana Figueres, Katibu Mtendaji wa mkataba wa kimataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi, UNFCCC, ametangaza hayo alipozungumza na waandishi wa habari leo mjini Geneva.

Audio Duration
59"

Lugha ya Kiswahili yazidi kuenea kwenye medani za kimataifa

Kwa mara ya kwanza ripoti ya Maendeleo ya binadamu inayoandaliaw na shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa imekuwa na muhtasari wake katika lugha ya Kiswahili. Uzinduzi wa muhtasari huo ulifanyika Kilifi, Mombasa Kenya tarehe 12 mwezi huu wa Juni na siku ya Alhamisi ya tarehe 20 Juni mjini New York Marekani, ubalozi wa Kenya ukafanya uwasilishaji wa muhtasari huo. Je nini kilijiri? Ungana na Assumpta Massoi katika makala hii ya wiki.

STUDIO: ASSUMPTA pckg

Miaka 50 ya Umoja wa Afrika umeshuhudia mafanikio: Ban

Umoja wa Mataifa unajivunia kuendelea kushirikiana na Umoja wa Afrika na wakazi wa bara hilo katika kuweka mazingira ya fursa na matumaini kwa wote, ni ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon hii leo tarehe 25 Mei, ambapo Umoja wa Afrika uliotokana na Umoja wa nchi huru za Afrika, OAU unatimiza miaka 50 tangu kuanzishwa kwake.  Amesema wakati waafrika wanakumbuka waasisi na magwiji wa karne ya 20 waliojitolea kwa hali na mali kupigania ukombozi na Umoja, ni wakati muhimu pia kuwa na matarajio ya zama za ustawi na amani.

Athari za teknohama zaangaziwa Geneva

Wakati dunia itaadhimisha siku ya kimataifa ya Jamii habari tarehe 17 mwezi huu, wawakilishi wa nchi wanachama wa Taasisi ya kimataifa ya mawasiliano ITU, taasisi za kimataifa, na wawakilishi wa Umoja wa Mataifa wanamkutana mjini Geneva, Uswisi, katika mkutano wa siku tatu unaolenga kuchukua mrejesho wa  lengo lililowekwa na wanachama hao la kuhakikisha dunia inafaidika na Jamii Habari ifikapo mwaka 2015. Mkutano huo ambao pia utaangazia athari za matumizi mabaya ya teknolojia ya habari na mawasiliano , Teknohama, na namna ya kuzikabili, utatumia miongozo iliyotolewa kwa kila nchi

Zebaki ni tishio kwa afya ya binadamu

Madini ya zebaki yana umuhimu mkubwa kwa maisha ya kila siku ya mwanadamu, lakini madini haya pia yametajwa kuwa na athari nyingi za afya ya mwanadamu kwa miaka mingi pasipo wengi kufahamu athari zake.

Utafiti unaonyesha kuwa viwango vya zebaki duniani vinaendelea kuongezeka vikichochewa kila siku za shughuli za mwanadamu zikiwemo uchomaji wa makaa ya moto na uchimbaji wa madini ya dhahabu. Zebaki huingia majini na kisha kuingia kwenye mwili wa binadamu kupitia ulaji wa samaki waliovuliwa kwenye maji hayo yenye madini ya Zebaki.