Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Serikali zafikia makubaliano kuhusu mabadiliko ya tabianchi

Serikali zafikia makubaliano kuhusu mabadiliko ya tabianchi

Pakua

Zaidi ya nchi 190 zimefikia makubaliano juu ya mazungumzo ya mabadiliko ya tabianchi.

Makubaliano hayo yamefikiwa baada ya siku saba ya mazungumzo nchini Uswisi, katika utaratibu wa maandalizi ya kongamano kubwa litakalofanyika mjini Paris, Disemba mwaka huu.

Christiana Figueres, Katibu Mtendaji wa mkataba wa kimataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi, UNFCCC, ametangaza hayo alipozungumza na waandishi wa habari leo mjini Geneva.

“ Ni lazima makubaliano ya Paris yaende sambamba na sayansi. Inamaanisha vitu viwili, kwanza tutatengeneza takwimu za awali, na pia tutaanzisha utaratibu wa muda mrefu kwa msingi wa kutorudi nyuma, na kuendelea kuchukua hatua zaidi hadi nusu ya pili ya karne hii”

Akizungumzia nafasi ya nchi zinazoendelea katika mkutano huo mwakilishi wa Tanzania katika ofisi za Umoja wa Matifa mjini Geneva Modest Mero anasema.

(SAUTI ya Mero)

Audio Duration
59"
Photo Credit
barafu zinazoyayuka, maeneo ya Alaska, nchini Marekani. Picha ya Camille Seaman/UNFCCC