Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Athari za teknohama zaangaziwa Geneva

Athari za teknohama zaangaziwa Geneva

Pakua

Wakati dunia itaadhimisha siku ya kimataifa ya Jamii habari tarehe 17 mwezi huu, wawakilishi wa nchi wanachama wa Taasisi ya kimataifa ya mawasiliano ITU, taasisi za kimataifa, na wawakilishi wa Umoja wa Mataifa wanamkutana mjini Geneva, Uswisi, katika mkutano wa siku tatu unaolenga kuchukua mrejesho wa  lengo lililowekwa na wanachama hao la kuhakikisha dunia inafaidika na Jamii Habari ifikapo mwaka 2015. Mkutano huo ambao pia utaangazia athari za matumizi mabaya ya teknolojia ya habari na mawasiliano , Teknohama, na namna ya kuzikabili, utatumia miongozo iliyotolewa kwa kila nchi ili kutimiza azma ya kunufaisha dunia katika sekta ya habari na mawasiliano.  Akizungumza katika mahojiano maalum na Radio ya Umoja wa Mataifa kutokaGeneva,  mmoja wa wakilishi waTanzaniakwenye mkutano huo Koni Shirima amesema nchi za Afrika zimetoa shuhuda mbalimbali juu ya namna zilivyotekeleza azhma hiyo akitolea mfano wa Rwanda ambayo imepiga hatua katika matumizi ya teknolojia ya kompyuta.

 (SAUTI KONI FRANCIS)