Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Radio ni muhimu sasa kuliko wakati wowote ule!

Radio ni muhimu sasa kuliko wakati wowote ule!

Pakua

Kuingia kwa zama za Televisheni kwa baadhi ya watu kulionekana kuwa mwanzo wa kuporomoka kwa usilizaji wa Radio. Lakini fikra hizo zimeonekana kuwa potofu kwa kuwa bado Radio inasikilizwa na watu wengi zaidi kuliko televisheni.

Radio bado ina umuhimu wake na ndio maana Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilitangaza tarehe 13 Februari ya kila mwaka kuwa ni siku ya Radio duniani. Je nini umuhimu wa siku hii? na matangazo ya Radio ya Umoja wa mataifa kwa sasa? Bi, Edda Sanga, mmoja wa watangazaji wakongwe wa Radio nchini Tanzania, kwa sasa ni Meneja wa vyombo vya habari vya Shule Kuu ya Uandishi wa Habari ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam, nchini Tanzania.

Katika mahojiano yake na Assumpta Massoi wa Radio ya Umoja wa Mataifa ameeleza kuwa kitendo cha kuwa na siku ya Radio duniani ni uamuzi sahihi na kwamba umuhimu wa Radio kwa sasa ni mkubwa zaidi kuliko wakati wowote ule.