Matukio ya mwaka 2017
Mwaka 2017 umefikia ukingoni! Kwa Umoja wa Mataifa mwaka huu ulianza na uongozi mpya wa Katibu Mkuu Antonio Guterres akiwa amepokea kijiti na kusema bayana kuwa hali si shwari. Na bila shaka hali ilikuwa hivyo mizozo kila kona na majanga ya asili nayo yakishika kasi. Umoja wa Mataifa ulikabiliwa na changamoto katika masuala ya amani, ulinzi na kibinadamu. Tunatumia fursa hii kuangazia mwaka huu unaomalizika wakati tukisubiri kwa hamu mwaka 2018. Wenyeji wako kwenye Jarida hili maalum ni Leah Mushi na Joseph Msami.