Umoja wa Mataifa na jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi ECOWAS leo wamelaani machafuko nchini Niger kufuatia tangazo la matokeo ya awali ya duru ya pili ya uchaguzi wa rais tarehe 21 Februari.
Maisha na mustakbali wa watoto zaidi ya milioni 3 waliotawanywa nchini Jasmhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, uko hatari huku dunia ikiwapa kisogo kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF.
Wakati serikali na mamilioni ya wananchi wa Uganda wakijiandaa kushiriki uchaguzi mkuu wa Rais na wabunge unaotarajiwa kufanyika kesho Alhamisi Januari 14, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametoa wito kwa wadau wote nchini humo kuhakikisha demokrasia inachukua mkondo.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema ameshtushwa na hali iliyoendelea leo mjini Washington DC nchini Marekani na kuwataka viongozi wa kisiasa kuwaasa wafuasi wao kujizuia na ghasia.
Wataalam huru wa hali za binadamu wa Umoja wa Mataifa leo wametoa wito kwa mamlaka ya Uganda kukomesha vitendo vya kuwakamata, kuwasweka rumande na kuwadhalilisha wapinzani wa kisiasa, viongozi wa asasi za kiraia na watetezi wa haki za binadamu.
Katika mkesha wa uchaguzi mkuu nchini Jamhuri ya Agfrika ya Kati CAR, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametoa wito kwa wadau wote kuhakikisha uchaguzi wa kesho Jumapili unafanyika kwa njia ya amani, uwe jumuishina wa kuaminika.
Mapigano na mivutano iliyoshuhudiwa wiki iliyopita nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR, ina athari kubwa kwa ulinzi wa raia nchini humo limeonya shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema anafuatilia kwa karibu hali inayoendelea hivi sasa nchini Uganda na kusema anatiwa hofu na ripoti za machafuko na mauaji kufuatia maandamano yanayofanyika mjini Kampala.