Vijana 700 wakuna vichwa kuhusu hatma ya SDG’s:
Kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, kumeanza jukwaa la vijana kutoka nchi wanachama wa umoja huo, wakiweka bayana kile wanachoona ni muhimu kwa mustakhbali wao.
Ukatili dhidi ya wakawake marufuku Burundi: Seruka
Ukatili wa kijinsia ni changamoto kubwa nchini Burundi huku Zaidi ya asilimia 90 ya wanaotendewa ukatili huo wakiwa ni wanawake na watoto. Sasa shirika lisilo la kiserikali la SERUKA limeamua kushikia bango dhuluma hiyo kwa kuendesha kampeni katika maeneo mbalimbali nchini humo kupinga na kuelimisha jamii kuachana na ukatili dhidi ya wanawake. Mwandishi wetu wa maziwa makuu Ramadhan Kibuga alitembelea moja ya kampeni za shirika hilo kwenye uwanja wa Parke mjini Bujumbura uangana naye kwenye Makala hii.
Habari za UN- Mtazamo wa kimataifa; Habari za kiutu
Pata muhtasari wa kile kitakachokuwemo katika wavu wetu mpya utakaozinduliwa rasmi tarehe 01 Februari mwaka huu wa 2018. Halikadhalika fahamu sababu za kuleta wavuti huu mpya. Wenyeji wako ni Flora Nducha na Siraj Kalyango.
Habari za UN- Mtazamo wa kimataifa; Habari za kiutu
Kunani?
Wavuti wa Radio ya Umoja wa Mataifa unafungwa rasmi mwishoni mwa mwezi Januari 2018. Nafasi yake itachukuliwa na ukurasa mpya ambao tuna imani utawapatia wasikilizaji na washirika katika vituo mbali mbali vya radio duniani, taarifa bora zaidi katika muundo tofauti.
Idara ya Habari kwa Umma ya Umoja wa Mataifa inayo furaha kuzindua wavuti huo ambamo kwao utapata taarifa katika mifumo yote. Mabadiliko haya kutoka Radio ya Umoja wa Mataifa hadi Habari za UN ni matokeo ya tafiti za kina kuhusu matumizi na mahitaji ya hadhira yetu.
Watu millioni 2.7 bado wakabiliwa na njaa kali Somalia
Uzalishaji wa chakula pamoja na vyanzo vya mapato vingi nchini Somalia vinatarajiwa kusalia chini kuliko kawaida katika maeneo mengi nchini humo.
Watu millioni 2.7 bado wakabiliwa na njaa kali Somalia
Uzalishaji wa chakula pamoja na vyanzo vya mapato vingi nchini Somalia vinatarajiwa kusalia chini kuliko kawaida katika maeneo mengi nchini humo.
Hii ni kutokana na uhaba mkubwa wa mvua za msimu za Oktoba- Disemba mwaka 2017 katika maeneo mengi ya Somalia huku mvua za msimu wa April hadi Juni zikitabiriwa nazo kuwa za kiwango cha chini.
Mvua zinazosaidia uzalishaji chakula nchini humo ni za aina mbili Deyr na Ga. Msimu wa Deyr hutokea katika miezi ya Oktoba hadi Disemba kila mwaka na ule wa Ga unaanza Aprili hadi Juni kila mwaka.
Hema linalohimili mabadiliko ya tabia nchi ni nuru kwa wakimbizi Uganda
Wakimbizi wa Sudani Kusini waishio kwenye makazi ya wakimbizi ya Maaji -Adjuman kaskazini mwa Uganda sasa wananeemeka na huduma ya afya kupitia hema maalumu linalohimili mabadiliko ya tabia nchi. Hema hilo la aina yake duniani limetolewa kama zawadi kwa wakimbizi hao na wanafunzi wa chuo kikuu cha Makerere baada ya hema hilo kuwawezesha kushinda tuzo ya ubunifu wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi. Kwa maelezo zaidi tuungane na Siraj kalyango
Mabilioni yapotea kwa kutotumia vizuri mikataba ya biashara huru, FTAs
Ripoti mpya iliyotolewa leo imeonyesha kuwa bado kuna shida kubwa katika matumizi sahihi ya mikataba ya biashara huria ambayo Muungano wa Ulaya imetia saini na nchi zingine.
Matumizi yasiyotosheleza ya mikataba hiyo husababisha kupotea kwa dola takribani bilioni 89, imesema ripoti hiyo iliandaliwa kwa pamoja na kamati ya biashara na maendeleo ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD na bodi ya taifa ya biashara ya Sweden.