Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na mkuu wa ujumbe wa Umoja huo nchini Libya UNSMIL, Ghassan Salame amesema kuwa mapigano baado yanaendelea katika mji wa Derna ulioko mashariki mwa taifa hilo.
Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya kibinadamu na msaada wa dharura, Ursula Mueller, amesema hali bado ni tete nchini Syria kufuatia mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yaliyodumu kwa zaidi ya miaka saba sasa.
Pata muhtasari wa kile kitakachokuwemo katika wavu wetu mpya utakaozinduliwa rasmi tarehe 01 Februari mwaka huu wa 2018. Halikadhalika fahamu sababu za kuleta wavuti huu mpya. Wenyeji wako ni Flora Nducha na Siraj Kalyango.
Umoja wa Mataifa umesema uko tayari kusaidia nchi za Asia ya Kati zinapoimarisha ushirikiano baina yao na Afghanistan ili kufanikisha malengo ya amani, maendeleo endelevu, utulivu na usalama.
Tishio la matumizi ya silaha za maangamizi linaongezeka kila uchao licha ya juhudi za kimataifa za kudhibiti na hatimaye kutokomeza matumizi ya silaha hizo.