Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari za wiki

Kipindupindu cha katili maisha Malawi

Watu watatu  wamefariki  dunia na wengine 196 kurepotiwa kuwa mahtuti  hadi katikati ya mwezi huu kufuatia  mlipuko wa kipindipindu katika sehemu za kaskazini mwa Malawi.

Tangu mlipuko huo utokee  juhudi  kadhaa zimekuwa zikifanywa na serikali  pamoja na mashirika mengine ya msaada kama vile la afya dunaini la WHO kuweza kukabiliana na mlipuko huo  hususan katika wilaya ya Karonga inayopakana na Tanzania.

Hali ya kibinadamu Syria bado ni mateso matupu- Mueller

Msaidizi wa Katibu  Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya kibinadamu na msaada wa dharura, Ursula Mueller, amesema hali bado ni tete nchini Syria kufuatia mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yaliyodumu kwa zaidi ya miaka saba sasa.

Katika taarifa yake kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hii leo kuhusu Syria, Bi. Mueller amesema mgogoro huo umesababisha mateso makubwa  kwa wananchi, vifo vingi kwa raia na huku wengine wakijeruhiwa au kutojulikana waliko.