Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Environment

Kipindupindu cha katili maisha Malawi

Watu watatu  wamefariki  dunia na wengine 196 kurepotiwa kuwa mahtuti  hadi katikati ya mwezi huu kufuatia  mlipuko wa kipindipindu katika sehemu za kaskazini mwa Malawi.

Tangu mlipuko huo utokee  juhudi  kadhaa zimekuwa zikifanywa na serikali  pamoja na mashirika mengine ya msaada kama vile la afya dunaini la WHO kuweza kukabiliana na mlipuko huo  hususan katika wilaya ya Karonga inayopakana na Tanzania.

Ukatili dhidi ya wakawake marufuku Burundi: Seruka

Ukatili wa kijinsia ni changamoto kubwa nchini Burundi huku Zaidi ya asilimia 90 ya wanaotendewa ukatili huo wakiwa ni wanawake na watoto. Sasa shirika lisilo la kiserikali la SERUKA limeamua kushikia bango dhuluma hiyo kwa kuendesha kampeni katika maeneo mbalimbali nchini humo kupinga na kuelimisha jamii kuachana na ukatili dhidi ya wanawake. Mwandishi wetu wa maziwa makuu Ramadhan Kibuga alitembelea moja ya kampeni za shirika hilo kwenye uwanja wa Parke mjini Bujumbura uangana naye kwenye Makala hii.

Habari za UN- Mtazamo wa kimataifa; Habari za kiutu

Kunani?

Wavuti wa Radio ya Umoja wa Mataifa unafungwa rasmi mwishoni mwa mwezi Januari 2018. Nafasi yake itachukuliwa na ukurasa mpya ambao tuna imani utawapatia wasikilizaji na washirika katika vituo mbali mbali vya radio duniani, taarifa bora zaidi katika muundo tofauti.

Idara ya Habari kwa Umma ya Umoja wa Mataifa inayo furaha kuzindua wavuti huo ambamo kwao utapata taarifa katika mifumo yote. Mabadiliko haya kutoka Radio ya Umoja wa Mataifa hadi Habari za UN ni matokeo ya tafiti za kina kuhusu matumizi na mahitaji ya hadhira yetu.

Watu millioni 2.7 bado wakabiliwa na njaa kali Somalia

Uzalishaji wa chakula pamoja na vyanzo vya mapato vingi nchini Somalia vinatarajiwa kusalia chini kuliko kawaida  katika maeneo mengi nchini humo.

Hii ni kutokana  na uhaba mkubwa wa mvua za msimu za Oktoba- Disemba mwaka 2017 katika maeneo mengi ya Somalia huku mvua za msimu wa April hadi Juni  zikitabiriwa nazo kuwa za kiwango cha chini.

Mvua zinazosaidia uzalishaji chakula nchini humo ni za aina mbili  Deyr na Ga. Msimu wa Deyr hutokea katika miezi ya Oktoba hadi Disemba kila mwaka na  ule wa Ga unaanza  Aprili hadi Juni kila mwaka.