Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari za UM

28 AGOSTI 2023

Hii leo jaridani jaridani tunaangazia hali ya usalama nchini Zimbabwe baada ya uchaguzi na masuala ya afya nchini Botswana. Makala tunakupeleka nchini Mali na mashinani nchini Rwanda, kulikoni?

Sauti
10'12"

25 AGOSTI 2023

Hii leo jaridani jaridani tunaangazia haki za binadamu nchini Sudan na utaifa wa Wapemba nchini Kenya. Makala tunakupeleka nchini Pakistan na mashinani nchini Tanzania, kulikoni?

Sauti
9'56"
UN/Anold Kayanda

Wanawake wapatiwe nafasi katika sayansi na teknolojia, watasongesha agenda 2030- Mwanaisha Ulenge

Ikiwa imesalia takribani miaka 6 ushehe kufika mwaka 2030 muda ambao ulimwengu ulijiwekea lengo la kuwa umetimiza Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs), mapema mwaka huu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akiamini wanawake wanasayansi wana uwezo wa kuchangia haraka katika maendeleo ya ulimwengu, alieleza namna kuwanyima fursa za sayansi wanawake kunarudisha maendeleo nyuma na hivyo akashauri wanawake wanasayansi wapewe nafasi kuanzia darasani, maabara na katika vyumba vya maamuzi.

Sauti
7'17"

22 AGOSTI 2023

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo Mapigano yanayoendelea huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC yakiendeshwa na vikundi vilivyojihami vya waasi yanaendelea kufurusha watu kutoka makwao, na hivyo wakimbizi hao wa ndani kushindwa kujikimu maisha yao ya kila siku. Malazi ni shida, makazi ni shida, halikadhalika chakula. Maisha yanakuwa ni changamoto kila uchao. Hali hiyo iko dhahiri kabisa jimboni Kivu Kaskazini ambako hata hivyo hatua za shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula duniani, WFP kwa wakimbizi Oicha zimeleta ahueni.

Sauti
9'59"

21 AGOSTI 2023

Hii leo jaridani tunaangazia Siku ya waathirika wa ugaidi duniani na mabomu ya kutegwa ardhini. Makala tunakupeleka nchini Siarra Leone na mashinani nchini Msumbiji, kulikoni? 

Sauti
9'56"
11-08-2023_DRC_Youth_Unemployment_Amani.JPG

Kijana Florent: Vijana DRC tunahaha kujikwamua kiuchumi lakini usalama unatukwamisha

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, vijana kesho wataadhimisha siku yao duniani huku kiza kinene cha ukosefu wa usalama kikiwa kimetanda mashariki mwa taifa hilo la ukanda wa Maziwa Makuu barani Afrika. Wakati Umoja wa Mataifa ukipigia chepuo vijana kushika hatamu ya kusongesha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs ikiwemo hatua kwa tabianchi, kutokomeza umaskini na ajira zenye hadhi, kwa vijana wa mashariki mwa DRC vuguvugu hilo linakumbwa na kikwazo cha usalama hata kama wawe wamepata elimu.

Sauti
4'26"

11 AGOSTI 2023

Hii leo jaridani tunaangazia Siku ya Vijana Duniani ambayo inaadhimishwa tarehe 12 Agosti 2023 kila mwaka na tutafuatilia kazi za vijana waliorejea nyumbani Gambia kutoka Ulaya. Pia tuanaangazia msaada wa kibinadamu Sudan. Makala tunakupeleka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na mashinani Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, salía papo hapo!

Sauti
12'10"