Kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, kumeanza jukwaa la vijana kutoka nchi wanachama wa umoja huo, wakiweka bayana kile wanachoona ni muhimu kwa mustakhbali wao.
Wakimbizi wa Sudani Kusini waishio kwenye makazi ya wakimbizi ya Maaji -Adjuman kaskazini mwa Uganda sasa wananeemeka na huduma ya afya kupitia hema maalumu linalohimili mabadiliko ya tabia nchi.
Ripoti mpya iliyotolewa leo imeonyesha kuwa bado kuna shida kubwa katika matumizi sahihi ya mikataba ya biashara huria ambayo Muungano wa Ulaya imetia saini na nchi zingine.
Pata muhtasari wa kile kitakachokuwemo katika wavu wetu mpya utakaozinduliwa rasmi tarehe 01 Februari mwaka huu wa 2018. Halikadhalika fahamu sababu za kuleta wavuti huu mpya. Wenyeji wako ni Flora Nducha na Siraj Kalyango.
Mkutano wa kawaida wa 30 wa viongozi wa Afrika ukiendelea huko Addis Ababa, Ethiopia, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametaja mambo matano ya kuimarisha ushirikiano ka