UNHCR yasaka dola milioni 157 kusaidia wahanga wa Boko Haram
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, pamoja na washirika wake katika juhudi za kutoa misaada ya kibinadamu, leo limezindua harambee ya kuchangisha dola millioni 157 kusaidia watu zaidi ya robo millioni ambao wameathirika na mashambulizi ya kundi la Boko Haram katika eneo la bonde la ziwa Chad.