Lazima tutambue changamoto za Kaskazini mwa Nigeria ili tuweze kuleta matumaini:Guterres
Changamoto kubwa zinazokabili jimbo la kaskazini mashariki mwa Nigeria la Borno, ambazo ni pamoja na ugaidi, zinahitaji kutambuliwa na jumuiya ya kimataifa ili kuunda kile ambacho Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amekiita "hali ya matumaini na hali halisi," katika eneo ambalo amesema halikufikia kilele cha sifa yake ya ugaidi, vurugu, kufurusha watu makwao au kukata tamaa.