Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya kibinadamu na msaada wa dharura, Ursula Mueller, amesema hali bado ni tete nchini Syria kufuatia mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yaliyodumu kwa zaidi ya miaka saba sasa.
Kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, kumeanza jukwaa la vijana kutoka nchi wanachama wa umoja huo, wakiweka bayana kile wanachoona ni muhimu kwa mustakhbali wao.
Ripoti mpya iliyotolewa leo imeonyesha kuwa bado kuna shida kubwa katika matumizi sahihi ya mikataba ya biashara huria ambayo Muungano wa Ulaya imetia saini na nchi zingine.
Pata muhtasari wa kile kitakachokuwemo katika wavu wetu mpya utakaozinduliwa rasmi tarehe 01 Februari mwaka huu wa 2018. Halikadhalika fahamu sababu za kuleta wavuti huu mpya. Wenyeji wako ni Flora Nducha na Siraj Kalyango.
Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kumbukizi ya wahanga wa mauaji ya halaiki dhidi ya wayahudi, Umoja wa Mataifa umesema silaha pekee dhidi ya vitendo kama hivyo ni elimu na uelewa kuhusu maadili ya kibinadamu.
Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Libya, amezindua mkakati wa kushughulikia zahma ya kibinadamu mwaka huu wa 2018 nchini Libya.
Mataifa yenye maendeleo duni zaidi duniani yako mbioni kumudu kuwa na mtandao wa mawasiliano ya intaneti ifikapo mwaka 2020 kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo.
Mataifa yenye maendeleo duni zaidi duniani yako mbioni kumudu kuwa na mtandao wa mawasiliano ya intaneti ifikapo mwaka 2020 kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo. Ripoti hiyo iliyotolewa na muungano wa kimataifa wa mawasiliano ITU inasema nchi zenye maendeleo duni au LDC’s zinapiga hatua kubwa katika kufikia fursa ya habari na teknolojia ya mawasiliano.