Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Funga mwaka yaingia na neema kwa wakimbizi Sudan Kusini

Malori ya misaada ya kibinadamu baada ya kuwasili katika mji wa Aweil, Sudan Kusini.

Funga mwaka yaingia na neema kwa wakimbizi Sudan Kusini

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP, limefurahishwa na hatua ya malori yake 30 yaliyosheheni chakula na misaada mingine ya kibinadamu kufika mji wa Aweil nchini Sudani Kusini. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.

(Taarifa ya Assumpta Massoi)

WFP kupitia mtandao wake wa Twitter imesema malori hayo yamesheheni tani 800 za chakula kama vile mahindi, soya mafuta ya kupikia na mahitaji mengine mbalimbali kwa ajili ya wakimbizi.
Kilichofurahisha zaidi ni kwamba misaada imefika muda muafaka wakati wa sherehe za kufunga mwaka. 
Mwezi uliopitam, msafara wa misaada wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF ulishambuliwa na makundi ya wahalifu na kusababisha uharibifu mkubwa wa misaada ya kibinadamu iliyohokuwa  imelenga wahitaji wakubwa ambao ni  wanawake na watoto.
 
WFP imekuwa ikiendesha shughuli za kibinadamu Sudan Kusini katika mazingira  hatarishi kutokana na hali ya usalama hasa wakati wa kusafirisha misaada ya kibinadamu.