Ukweli kuhusu dhana nne potofu kuhusu usalama wa mtoto mtandaoni
Maisha ya watoto na vijana kwa muda mrefu yameunganishwa na intaneti na mitandao ya kijamii na kadri teknolojia inavyoendelea kubadilika kwa kasi jambo hili linaongezeka na kuenea zaidi na kuruhusu watoto kufikia ulimwengu wa habari, kujifunza, kushirikiana, burudani na zaidi inaweza kuwa chanya lakini wakati mwingine kuna hatari, linaeleza shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF katika makala hii iliyochapishwa kwenye wavuti wa shirika hilo leo Siku ya Kimataifa ya intaneti salama.