wanawake

Takribani nusu ya wanawake wote katika nchi zinazoendelea, wananyimwa uhuru wao wa mwili: Ripoti ya UNFPA  

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu, UNFPA iliyotolewa leo Aprili 14, 2021, takribani nusu ya wanawake wote katika nchi 57 zinazoendelea wananyimwa haki ya kuamua kuhusu miili yao kama vile tendo la ndoa, uzazi wa mpango au kutafuta huduma za afya.

Mradi wa Benki ya Dunia Afghanistan wasaidia wanawake kuinua maisha yao 

Nchini Afghanistan, mradi wa pamoja wa Benki ya Dunia na wakfu wa ujenzi mpya wa taifa hilo, ARTF umesaidia wanawake kuweza kudai haki yao ya msingi ya kumiliki ardhi inayotambulika kisheria na sasa kuwawezesha wale wanaomiliki ardhi siyo tu kuwa na maisha bora zaidi bali pia thamani ya ardhi wanayomiliki kuongezeka kutokana na hatimiliki.

Wanawake Uganda wataka haki ya ardhi kwa kurekebisha sheria ya ndoa na talaka.

Lengo namba 5 la Malengo ya Umoja w mataifa ya maendeleo endelevu linaangazia usawa wa kijinsia likilenga kufanya mageuzi ili kuwapa wanawake haki sawa kwa rasilimali za kiuchumi, na pia kupata umiliki na udhibiti wa ardhi na aina nyingine za mali, huduma za kifedha, urithi na maliasili, kwa muji

Sauti -
4'10"

Kumekuwa na mafanikio lakini bado tunajikongoja kufikia usawa wa kijinsia:Guterres 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema miaka 26 baada ya mkutano wa nne wa kimataifa wa wanawake na usawa wa kijinsia , hatua kubwa zimepigwa na mafanikio yameonekana lakini bado dunia inajikongoja kutimiza azimio la Beijing na hatua za kufikia usawa wa kijinsia. 

Asilani hakuna mwanangu atakaye keketwa! 

Kama asilimia 95 ya wanawake wanawake katika jamii yake chini Uganda, wamekeketwa. Margaret Chepoteltel alikeketwa  (FGM) utotoni na kutumbukia katika madhara ya kiafya katika maisha yake yote.  

Mwanamke, kwenye uongozi huletewi kadi kama harusi - Balozi Getrude Mongela.

Mwanamke, kwenye uongozi huletewi kadi kama harusi - Balozi Getrude Mongela.

Sauti -
6'44"

Mwanamke, kwenye uongozi huletewi kadi kama harusi - Balozi Getrude Mongela

Kikao hiki cha 65 cha kamisheni ya hali ya wanawake duniani kilichoanza tarehe 15 Machi kikiwa sasa kinakamilisha wiki yake ya kwanza, wadau kwa namna mbalimbali kote duniani wanaendelea kujadili mada ya mwaka huu ambayo imejikita kwenye kuangazia wanawake katika uongozi ili kufikia dunia yenye u

Sauti -
6'42"

Ni wakati wa kuhakikisha mwanamke anashika usukani kila nyanja Guterres akiambia kikao cha CSW65

Mkutano wa kamisheni ya hali ya wanawake  duniani kikao cha 65 umefungua pazia hii leo ikiwa ni mara ya pili kufanyika katika mazingira ya janga la virusi vya corona au covid-19 ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema janga hili lina sura ya mwanamke akisema kwamba hali ya sasa imedhihirisha jinsi ukosefu wa usawa wa kijinsi ulivyo kwa kiasi kikubwa na umekita mizizi katika mifumo ya kisiasa, kijamii na kiuchumi. 

15 Machi 2021

Jaridani Machi 15 2021 na Grace Kaneiya kwa habari kwa ufupi, makala yetu kwa kina ikiangazia mwanamke kiongozi na ujumbe kutoka kwa Mkurugenzi mtendaji wa UN-HABITAT.

Sauti -
11'24"

09 Machi 2021

Hii leo jaridani Flora Nducha anamulika harakati za kuondokana na ndoa za umri mdogo duniani akimulika mtoto aliyeolewa na mzee huko nchini Bangladesh, kisha anaangazia mpango wa elimu haiwezi kusubiri ambao umepatiwa dola milioni 1 nchini Niger na mwisho ni taarifa kuhusu madereva wanawake nchin

Sauti -