Tusiwasahau wakimbizi wa Congo na shida wanazopitia UNHCR/ CHRISTINA
Msanii mashuhuri wa Ufaransa Christine pamoja na kundi lake the Queens wametoa wito kwa mashirika ya kibinadamu na wahisani kutopuuzia suala la machafuko yanayoendelea Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo DRC na kusababisha wimbi kubwa la wakimbizi wanaofungasha virago kila uchao.
Akitoa wito huo wakati alipotembelea kambi ya wakimbizi wa kutoka DRC walioko Kusini Magharibi mwa Uganda , Christina amesema anajaribu kutumia nafasi yake kama msanii wa muziki na pia mtu mashuhuri kupaza sauti kwa jamii ya kimataifa na wahisani kutosahau zahma wanazopitia wakimbizi.
Katika ziara yake hiyo Christina alipatafursa ya kutemebelea pia kituo cha mafunzo kwa vijana wakimbizi cha Rwamwanja kilichopo chini ya usimamizi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na kusema amefurahiswa na jitiahda za UNHCR kuwapa vijana fursa ya kijifunza muziki na pia michezo mbalimbali wakiti wakiwa katika hali ngumu kambini.
Bwana Bornwell kantande ambaye ni mwakilishi wa UNHCR nchini Uganda amesema nchini hiyo inahifadhi zaidi ya wakimbizi milioni 1.4 kutoka ukanda wa Afrika Mashariki kama Burundi,Sudan kusini, na zaidi ya laki 230 wanatoka DRC.