Skip to main content

Chuja:

vita

25 SEPTEMBA 2023

Hii leo jaridani tunaangazia machafuko nchini Ukraine na mkutano wa kimataifa huko Rome kuhusu marekebisho ya mfumo wa ufugaji wa wanyama. Makala tunasalia hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa na mashinani tunakupeleka nchini Poland, kulikoni?

Sauti
12'56"

08 SEPTEMBA 2023

Hii leo jaridani tunaangazia habari za masikitiko kuhusu watototo katika migogoro nchini DRC. Pia tunamulika pengo katika usawa wa kijinsia.  Makala tunarejelea ufafanuzi wa ibara ya 9 ya Tamko la Umoja wa Mataifa la haki za binadamu na mashinani tunakuletea ujumbe wa vijana kuhusu mabadiliko ya tabianchi.

Sauti
11'22"
© UNICEF/Ahmed Elfatih Mohamdee

Griffiths: Vita na njaa vinaweza kusambaratisha Sudan

Vita inayoendelea nchini Sudan inachochea dharura kubwa ya kibinadamu ambapo vita na njaa, magonjwa na watu kufurushwa makwao vilivyofuatia sasa  inatishia ‘kutafuna’ nchi nzima, amesema Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu, OCHA, Martin Griffiths. 

Taarifa iliyotolewa na OCHA hii leo jijini New York, Marekani imemnukuu mkuu wa ofisi hiyo Martin Griffiths akisema kuwa mapigano makali yaliyoanzia mji mkuu wa Sudan, Khartoum na jimbo la Darfur katikati ya mwezi Aprili mwaka huu yamesambaa hadi Kordofan. 

Sauti
1'57"
11-08-2023_DRC_Youth_Unemployment_Amani.JPG

Kijana Florent: Vijana DRC tunahaha kujikwamua kiuchumi lakini usalama unatukwamisha

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, vijana kesho wataadhimisha siku yao duniani huku kiza kinene cha ukosefu wa usalama kikiwa kimetanda mashariki mwa taifa hilo la ukanda wa Maziwa Makuu barani Afrika. Wakati Umoja wa Mataifa ukipigia chepuo vijana kushika hatamu ya kusongesha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs ikiwemo hatua kwa tabianchi, kutokomeza umaskini na ajira zenye hadhi, kwa vijana wa mashariki mwa DRC vuguvugu hilo linakumbwa na kikwazo cha usalama hata kama wawe wamepata elimu.

Sauti
4'26"

11 AGOSTI 2023

Hii leo jaridani tunaangazia Siku ya Vijana Duniani ambayo inaadhimishwa tarehe 12 Agosti 2023 kila mwaka na tutafuatilia kazi za vijana waliorejea nyumbani Gambia kutoka Ulaya. Pia tuanaangazia msaada wa kibinadamu Sudan. Makala tunakupeleka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na mashinani Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, salía papo hapo!

Sauti
12'10"
UN News

OCHA: Maisha ya kila siku nchini Sudan ni jinamizi

Mkuu wa kitengo cha Operesheni na Uchechemuzi kwenye Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na masuala ya kibinadamu na kuratibu masuala ya dharura OCHA Edem Wosornu amesema maisha ya kila siku ya wananchi nchini Sudan yamegubikwa na sintofahamu kutokana na vita inayoendelea hivyo amesihi pande husika kukomesha mapigano na wakati huo huo wahisani waongeze ufadhili wa kibinadamu. 

Sauti
1'52"