Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

WFP

Mlo shuleni ni lengo kuu la WFP katika Jamhuri ya Congo.
© WFP/Gabriela Vivacqua

WFP yataka uwekezaji wa haraka kuzuia udumavu kwa watoto huku viongozi wakikutana kwenye mkutano wa lishe kwa ukuaji

Wakati viongozi wa dunia na wataalamu wanapokutana mjini Paris Ufaransa kwa ajili ya Mkutano wa nne wa Lishe kwa Ukuaji, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula Duniani WFP limetoa wito wa kuzingatia na kuchukua hatua zaidi ili kuzuia udumavu ambao ni aina mbaya zaidi ya utapiamlo kabla madhara yake hatari kwa maisha ya watoto hayajadhihirika likisema kuchukua hatua kabla ya utapiamlo kushika kasi ni jambo la msingi.

Hali katika kambi ya Al Mawasi kusini-magharibi mwa Gaza bado ni mbaya zaidi na haifai mamia ya maelfu ya watu wa Gaza walioondolewa na kuongezeka kufuatia ghasia karibu na Rafah na mahali pengine katika Ukanda wa Gaza.
UN News/Ziad Taleb

Uvamizi wa Israel ukiendelea Ukanda wa Gaza, vituo vya misaada vinafunga kimoja baada ya kingine: UN

Bila dalili ya yaliyoripotiwa mapigano mitaani na mashambulizi ya Israel Gaza leo, wahudumu wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa wameonya kwamba mtiririko wa msaada muhimu wa kuokoa maisha katika eneo hilo umepungua kwa zaidi ya theluthi mbili tangu jeshi la Israel liongeze operesheni yake huko Rafah na kunyakua ufunguo huo wa mtiririko wa misaada.

Takriban watu milioni 18 kote nchini Sudan wanakabiliwa na njaa kali.
Nearly 18 million people across Sudan are facing acute hunger.

Sudan iko ukingoni kukabiliwa na njaa

Miezi minane baada ya vita kuzuka nchini Sudan, Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na Shirika la Kilimo la Chakula na Kilimo (FAO) yameonya leo Ijumaa kuhusu "janga la njaa" katika nchi hiyo mwaka ujao ikiwa watashindwa kusaidia wakulima na kusambaza chakula kwa haraka kwa watu walionaswa katika maeneo kitovu cha vurugu.