17 MEI 2023
Jaridani hii leo tunaangazia machafuko nchini Sudan na mchakato wa uchaguzi nchini Sudan Kusini. Makala tunakupeleka nchini Kenya na Mashinani yunasalia hapa makao makuu kusikia ujumbe kuhusu idadi ya watu duniani.

Jumuiya ya kimataifa inapaswa kuangazia zaidi na kwa mwelekeo wa mkataba wa amani Sudan Kusini pamoja na ongezeko la ghasia miongoni mwa jamii nchini kote Sudan Kusini, wameonya wataalamu wa Umoja wa Mataifa wa haki za binadamu nchini humo baada ya kuhitimisha ziara yao jijini New York, Marekani ambako wamepata fursa ya kuzungumza na maafisa mbalimbali. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.
Nchini Sudan Kusini, watoto waliokuwa wametumikishwa vitani na hatimaye kuachiliwa huru sasa wameanza kubadili maisha yao na ya wengine baada ya kupatiwa stadi za kujipatia kipato kwa msaada wa Umoja wa Mataifa na wadau wake.
Wanawake, wasichana na Watoto nchini Sudan Kusini ndio wanaobeba gharama kubwa ya vita, huku maelfu wakipitia madhila ya kubakwa, utekaji, kunyimwa haki, kutawanywa na hata vifo. Lakini sasa wana fursa kubwa ya kuleta amani. John Kibego na tarifa kamili
Shirika la uhamiaji la Umoja wa Mataifa IOM leo mjini Juba nchini Sudan Kusini, limezindua ombi lake la mwaka huu wa 2019 la dola milioni 122 zinahitajika ili kuwasaidia takribani watu milioni 1 nchini Sudan Kusini hususani wale ambao wamepoteza makazi na kujikuta katika ukimbizi wa ndani pamoja na wale wanaorejea baada ya kuyakimbia machafuko.
Walinda amani Sudan Kusini wasindikiza wanafunzi shuleni na kuwarudisha nyumbani wakati wa mitihani.Polisi waliopo kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini wamepewa jukumu la kuwasindikiza wanafunzi hadi kwenye kituo cha mtihani kwenye mji mkuu wa Sudan Kusini, Juba. Usindikizaji huo unafanyika Kwa wiki mbili ambapo askari hao wataendelea kuwapeleka na kuwarudisha wanafunzi kufanya mitihani yao kwa usalama.
Bado ni alfajiri na kuna giza lakini polisi wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini wameshafika katika eneo la kukutania tayari kupata maelekezo ya siku.
Walinda amani Sudan Kusini wasindikiza wanafunzi shuleni na kuwarudisha nyumbani wakati wa mitihani.Polisi waliopo kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini wamepewa jukumu la kuwasindikiza wanafunzi hadi kwenye kituo cha mtihani kwenye mji mkuu wa Sudan Kusini, Juba. Usindikizaji huo unafanyika Kwa wiki mbili ambapo askari hao wataendelea kuwapeleka na kuwarudisha wanafunzi kufanya mitihani yao kwa usalama.
Amani ya kudumu na endelevu haitopatikana nchini Sudan Kusini endapo jamii hususan wanawake hawatoshirikishwa katika mchakato wa kuileta. Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa operesheni za ulinzi wa Umoja wa Mataifa Jean Pierre Lacroix baada ya kukutana na wanawake wakimbizi wa ndani kwenye eneo la Bentiu nchini humo.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan, Mohamed Ahmed Eldirdiri amehutubia mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na kusema kuwa mazingira ya sasa yanatia moyo katika kupatia suluhu masuala yote yaliyosalia kati ya nchi yake na Sudan Kusini.
Licha ya vita vinavyoendelea na changamoto nyingine lukuki nchini Sudan Kusini, Daktari mmoja bingwa wa upasuaji nchini humo amedhamiria kufanya kila awezalo kuokoa maisha ya maelfu ya wakimbizi wa ndani nchini humo, huku akifanya kazi katika mazingira magumu yaliyomfanya kutunukiwa tuzo ya wakimbizi mwaka huu.