Kenya

Mhitimu wa kidato cha 4 Kenya, Daniel Nderitu atengeneza redio na kusaidia watoto wakati wa COVID-19

Ubunifu, hususani wa vijana katika sayansi na teknolojia, ni moja ya mambo ambayo yanatajwa kuwa yatasaidia kusongesha lengo kuu la ufikiaji wa malengo 17 Umoja wa Mataifa ya maendeleo endevu, SDGs.

Sauti -

11 Februari 2021

Hii leo Jaridani Grace Kaneiya kutoka Nairobi Kenya anaanza Habari za UN akimmulika msichana kutoka Rwanda ambaye ni mhandisi wa magari kwenye kampuni ya magari ya Hyundai kwenye mji mkuu Kigali, ikiwa ni katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya wanawake na wasichana katika sayansi.

Sauti -
13'38"

05 Februari 2021

Leo Ijumaa ni mada kwa kina na Assumpta Massoi anakupeleka Nairobi Kenya ambako Grace Kaneiya katika kufuatilia utekelezaji wa mwaka wa kimataifa wa mboga mboga na matunda amevinjari kwa familia moja jijini Nairobi kuona mtazamo wao katika ulaji wa mboga za majani na matunda.

Sauti -
10'39"

04 Februari 2021

Hii leo jaridani Grace  Kaneiya kutoka Nairobi nchini Kenya anaanzia na taarifa kuhusu siku ya saratani duniani ikimulika changamoto za upimaji wa gonjwa hilo wakati huu wa janga la COVID-19.

Sauti -
13'25"

02 Februari 2021

Hii leo jaridani Flora Nducha anaanza na ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu usafirishaji haramu wa binadamu ikionesha kuwa wavulana wanaosafirishwa kiharamu idadi yao imeongezeka katika kipindi cha miaka miwili iliyopita. Watu wengine wanasafirishwa pia kutumikishwa kwenye kuombaomba.

Sauti -
13'59"

27 Januari 2021

Hii leo jaridani Flora Nducha anaanzia nchini Tanzania kumulika harakati za watoto wa kike na elimu, kisha anakukutanisha na wajasiriamali vijana kupitia shirika la maendeleo ya viwanda la Umoja wa Mataifa, UNIDO.

Sauti -
13'43"

Aweka faida kando kuunga mkono hoja ya UN ya afya kwa kila mtu

Afya bora ni moja ya malengo ya maendeleo endelevu, SDGs, ya Umoja wa Mataifa.

Mara nyingi mtu akianzisha biashara, mathalani ya kutoa huduma za hospitali, lengo huwa ni kutafuta faida na kujiendeleza na ni wachache mno wanaotumia biashara zao kunufaisha jamii bila malipo.

Sauti -
4'36"

26 Januari 2021

Hii leo jaridani Flora Nducha anaanzia Msumbiji ambako kimbunga Eloise kimetonesha kidonda cha manusura wa vimbunga Chalane na Idai. Kisha atabisha hodi Burkina Faso akimulika raia waliokimbia vurugu makwao wakikumbwa na janga la mabadiliko ya tabianchi.

Sauti -
13'6"

Ndizi zageuzwa unga huko Nyeri na sasa vijana wajipatia kipato- IFAD

Chukua vijana wajasiriamali, wapatie vifaa vya kisasa na mafunzo basi utakuwa umebadilisha maisha si ya kwao tu bali na jamii zao ,na hicho ndio kilichotokea huko Nyeri nchini Kenya baada ya Umoja wa Mataifa na serikali ya Kenya kushikana mikono na kunasua vijana ambao walikuwa kidoto wakate tama

Sauti -
2'19"

Vijana Nyeri Kenya waona nuru ya maisha kupitia usindikaji wa ndizi 

Chukua vijana wajasiriamali, wapatie vifaa vya kisasa na mafunzo basi utakuwa umebadilisha maisha si ya kwao tu bali na jamii zao ,na hicho ndio kilichotokea huko kaunti ya Nyeri nchini Kenya baada ya Umoja wa Mataifa na serikali ya Kenya kushikana mikono na kunasua vijana ambao walikuwa kidoto wakate tamaa.