Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, Filippo Grandi akiwa ziarani barani Afrika, ametembelea wanafunzi katika shule inayofanya vizuri zaidi kimasomo kwa wakimbizi na wenyeji nchini humo na akaongeza wito wa uwekezaji zaidi katika elimu kwa watu waliofurushwa na pia jamii zinazowakaribisha.