afrika

Kifo 1 kati ya 5 vya COVID-19 Afrika kinahusiana na kisukari:WHO 

Katika kuelekea siku ya kisukari duniani itakayoadhimishwa kesho Novemba 14, shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO limebaini kwamba kifo kimoja kati ya vitano vya corona au COVID-19 barani Afrika kinahusiana na ugonjwa wa kisukari.

Kando na madhila yatokanayo na COVID-19 kwa upande mwingine imetoa fursa ya ubunifu

Utafiti mpya wa Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa WHO uliotangazwa katika mji mkuu wa Jamhuri ya Congo, Brazzaville, umesema janga la

Sauti -
2'51"

COVID-19 inahimiza ubunifu wa kiafya barani Afrika-WHO

Utafiti mpya wa Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa WHO uliotangazwa katika mji mkuu wa Jamhuri ya Congo, Brazzaville, umesema janga la COVID-19 limeongeza nguvu kwenye maendeleo ya ubunifu zaidi ya 120 wa teknolojia ya afya ambao umejaribiwa au kupitishwa barani Afrika.

Tishio la mabadiliko ya tabianchi linaendelea kuongezeka Afrika:WMO Ripoti

Ripoti mpya iliyotolewa na shirika la Umoja wa utabiri wa hali ya hewa WMO ikitanabaisha hali ya sasa na mustakabali wa hali ya hewa katika bara la Afrika inaonyesha kwamba mwaka 2019 ulikuwa miongoni mwa miaka mitatu yenye joto la kupindikia katika historian a mwenendo unatarajiwa kuendelea  ukisababisha watu kutawanywa na athari katika kilimo. 

Wahamiaji wengi toka Afrika hawaendi Ulaya wala Amerika bali katika nchi za Afrika:IOM/AUC Ripoti 

Ripoti mpya na ya kwanza kabisa ya uhamiaji Afrika iliyotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM na tume ya Muungano wa Afrika AUC, imebaini kwamba wahamiaji wengi wa bara hilo hawaendi kwingineko bali barani mwao Afrika.

Huu ni wakati muhimu kwa vita dhidi ya COVID-19 kila kiongozi aongeze juhudi:Dkt. Tedros

Mkurugenzi mkuu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO Dkt. Adhanom Ghebreyesus leo amemtakia Rais wa Marekani Donald Trump na mkewake Melania Trump ahuweni na kupona haraka baada kupimwa na kugundulikwa kuwa wameambukizwa corona au COVID-19

Hatua tulizochukua dhidi ya COVID-19 zimedhihirishia ulimwengu uthabiti wetu Afrika 

Fikra za baadhi ya watu kuwa maelfu kwa maelfu ya watu barani Afrika watapukutika kutokana na janga la ugonjwa wa Corona, au COVID-19 zimekuwa ndivyo sivyo baada ya bara hilo kuchukua hatua kitaifa na kikanda na hatimaye hadi sasa kudhihirisha umuhimu wa mshikamano katika kukabili adui. Hilo limebainishwa wakati wa hotuba za marais waliohutubia mjadala mkuu wa mkutaon wa 75 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwa njia ya mtandao kutokana na vikwazo vilivyopo Marekani kutokana na janga la Corona. Flora Nducha anamleta Assumpta Massoi ambaye amefuatilia hotuba za viongozi hao na anaeleza kwa kina.

Nchi za Afrika zashiriki mkakati mkubwa wa chanjo ya COVID-19 :WHO 

Wakati mbio za kusaka chanjo salama na inayofanya kazi dhidi ya janga la corona au COVID-19 zikiendelea kote duniani, nchi za Afrika zinajisajili katika mkakati mkubwa wenye lengo la kupata takriban dozi milioni 220 za chanjo kwa ajili ya bara hilo pindi leseni ya chanjo hiyo itakapotolewa na kuidhinishwa. 

Kampeni za nyumba kwa nyumba, eneo kwa eneo zatokomeza Polio Afrika

Polio! Polio! Polio! Ugonjwa uliokuwa ukilemaza watoto 75,000 kila mwaka wakati wa miaka ya 1990 katika nchi za Afrika wanachama wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa kanda ya Afrika.

Sauti -
3'58"

Afrika yatokomeza Polio

Hatimaye nchi za Afrika zilizo kwenye ukanda wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO kwa kanda ya Afrika zimefanikiwa kutokomeza ugonjwa wa Polio.