Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UDHR70

UDHR70
Tamko la Haki za Binadamu la UN-Uchambuzi wa Ibara

Tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa, UDHR, ni nyaraka ya kihistoria iliyopitishwa na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa mwaka 1948 kwa lengo la kuhakikisha haki za binadamu zinalindwa. Rasimu ya nyaraka hii iliandaliwa na wawakilishi wenye usuli tofauti kuanzia sheria hadi utamaduni na walitoka maeneo yote ya dunia. Baada ya kuiandaa na kuijadili rasimu hiyo ilipitishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa tarehe 10 Disemba mwaka 1948 mjini Paris, Ufaransa kwa azimio namba 217 A la baraza hilo. Likipatiwa jina la tamko la haki za binadmu, nyaraka hiyo inaweka viwango vya pamoja vya haki za binadamu kwa wote na mataifa yote. Azimio hilo, kwa mara ya kwanza liliweka misingi ya haki za binadamu inayokubalika kimataifa na inayopaswa kulindwa popote pale duniani. Hadi sasa nyaraka hiyo imetafsiriwa kwa zaidi ya lugha 500 ikiwemo Kiswahili.

Pata taarifa kila wakati pindi tunapochapisha taarifa mpya kwa kujisajili

UNICEF/UN0153963/Obadi

Mkimbizi bila elimu ni sawa na mti bila matunda:Mkimbizi Rachel

Elimu kwa mkimbizi ni muhimu sana, kwani bila elimu huwezi fanya chochote , iwe ni kwa upande wa ajira au hata ujasiriliamali, unakuwa sawa na mti usiozaa matunda ambao huonekana kutokuwa na faida yoyote. Kauli hiyo ni ya mmoja wa wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidekrasia ya Congo DRC, ambaye aliishi na kusomea kambini nchini Uganda. Akizungumza na mwandishi wetu John Kibego kuhusu haki ya kila mtu kupata elimu bila kujali kabila, rangi au uraia wake kama ilivyoainishwa kwenye Ibara ya 26 ya tamko la haki za binadamu, anasema haijalishi mazingira uliyopo “elimu ni elimu”.

Sauti
3'32"
WFP/Jonathan Dumont

Serikali zina wajibu kuhakikisha wananchi wana makazi yenye staha.

Katika uchambuzi wa ibara kwa ibara za tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa, hii leo Assumpta Massoi anamulika ibara ya 15 ambayo inagusia haki ya msingi ya mtu kuishi maisha ya staha. Ibara hii inazingatia  ukweli kwamba baadhi ya maeneo licha ya sheria kutambua haki hiyo, bado maisha ya wananchi ni magumu, wakiishi maeneo yasiyo na staha, huduma za kijamii zikiwa ni mashakani. Na wakati mwingine, hata pale ambapo wananchi wamejinasua, wanakumbwa na ubomoaji ambao husababisha watumbukie tena kwenye mkwamo .Je hali inakuwa vipi na Umoja wa Mataifa unasema nini?

Sauti
3'22"
FAO/Giulio Napolitano

Ibara ya 24

Mapumziko na burudani ikiwemo kuwa na muda wenye ukomo wa kufanya kazi na pia kupatiwa likizo yenye malipo ni haki ya kila mtu kwa mujibu wa  Ibara ya 24 ya tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa linalotimiza miaka 70 mwezi huu. Lakini je haki hii ya msingi inatekelezwa vipi? Katika makala hii, Mwanasheria Tito Magoti wa kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC Tanzania akijadili na Arnold Kayanda anaanza kwa kueleza mantiki ya ibara yenyewe.

 

Sauti
2'11"
UN Picha/Greg Kinch

Hali ya baadhi ya wafanyakazi ughaibuni inasikitisha- Emma Mbura

Ibara ya 23 ya tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa inasema kila mtu ana haki ya kufanya kazi, kuchagua kazi anayoifanya, kufanya kazi katika mazingira salama na ulinzi dhidi ya ukosefu wa ajira. Kipengele cha pili kwenye ibara hiyo kinasema kuwa kila mtu, bila kubaguliwa ana haki ya kulipwa mshahara sawa kwa kazi sawa. Ibara hiyo inakwenda mbali zaidi na kusema kuwa kila mtu ana haki ya ujira unaofaa kwa ajili ya matumizi yake na familia kuwawezesha kuishi kwa utu na nyongeza kwa ajili ya ulinzi wa kijamii.

Sauti
5'14"