Pamoja na kustahili uhuru, kila mtu ana wajibu kwa jamii.

9 Disemba 2018

Tarehe 10 Desemba 1948, Umoja wa Mataifa uliridhia tamko la haki za binadamu ambalo kwa miaka yote limekuwa muongozo kwa nchi wanachama kote duniani kutunga sheria zinazolenga kumwakikishia haki kila mwanadamu, na kwa hivyo tarehe 10 Desemba mwaka huu wa 2018, dunia inaadhimisha kutimia kwa miaka 70 ya tamko hilo.

Kati ya ibara 30 zinazokamilisha tamko hilo, ibara ya 28 inasema, mosi, kila mtu ana wajibu kwa jamii ambamo kwayo ndio kunaweza kupatikana uhuru na maendeleo kamili ya hali bora ya maisha yake, pili katika kutumia haki na uhuru wake, kila mtu itambidi kufuata kanuni zile zilizowekwa na sheria kwa ajili ya kulinda heshima inayotakiwa juu ya haki na uhuru wa watu wengine, na kukidhi kanuni za haki, usalama na hali njema ya maisha katika jamii ya kidemokrasia na tatu uhuru huu na haki hizi kamwe visitumiwe kinyume na malengo na misingi ya Umoja wa Mataifa.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter