Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Serikali zina wajibu kuhakikisha wananchi wana makazi yenye staha.

Serikali zina wajibu kuhakikisha wananchi wana makazi yenye staha.

Pakua

Katika uchambuzi wa ibara kwa ibara za tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa, hii leo Assumpta Massoi anamulika ibara ya 15 ambayo inagusia haki ya msingi ya mtu kuishi maisha ya staha. Ibara hii inazingatia  ukweli kwamba baadhi ya maeneo licha ya sheria kutambua haki hiyo, bado maisha ya wananchi ni magumu, wakiishi maeneo yasiyo na staha, huduma za kijamii zikiwa ni mashakani. Na wakati mwingine, hata pale ambapo wananchi wamejinasua, wanakumbwa na ubomoaji ambao husababisha watumbukie tena kwenye mkwamo .Je hali inakuwa vipi na Umoja wa Mataifa unasema nini? Ungana basi na Assumpta Masso kwenye makala hii.

Audio Credit
Siraj Kalyango/Assumpta Massoi
Audio Duration
3'22"
Photo Credit
WFP/Jonathan Dumont