Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kila mtu ana haki ya kupata elimu. Kabila, rangi au uraia visiwe vikwazo.

Watoto wakiwa ndani ya darasa la shule ya hema ya UNICEF katika kambi ya Alhabanya,Anbar, Iraq.Watoto wahamiaji na wakimbizi hukosa elimu wanakokimbilia.
UNICEF/UN0161150/Anmar

Haki za binadamu

Uchambuzi wa  ibara  linalotimiza za tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa linalotimiza miaka 70 mwezi huu wa desemba 2018 unaendelea.

Katika Ibara ya 26 ya tamko la haki za binadamu imezizitizwa haki ya kila mtu kupata elimu, na kusoma kadri apendavyo bila kujali kabila , rangi au uraia. Ibara hiyo inaungwa mkono na mmoja wa wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, aliyesoma na kukulia kwenye kambi ya wakimbizi nchini Uganda. Akizungumza na mwandishi wetu John Kibego anasisitiza kwamba bila kujali mazingira uliyopo yawe ya ukimbizi ama la” elimu ni elimu” na ni ufunguo wa maisha.