Ibara kwa Ibara za Tamko la Haki za Binadamu

30 Oktoba 2018

Uchambuzi wa ibara za tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa

Kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 70 ya tamko la haki za binadamu duniani tarehe 10 mwezi disemba mwaka 2018, Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa inakuletea mfululizo wa uchambuzi wa Ibara 30 za tamko hilo.

Uchambuzi huo utafanyika kwa njia mbalimbali ikiwemo taarifa za habari zitakazohusisha wataalamu, bila kusahau makala, video na maoni kutoka mashinani kuhusu utekelezaji wa azimio hilo ambalo limetafsiriwa kwa lugha 512 ikiwemo Kiswahili.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter