Ushiriki na upatikanaji wa huduma za jamii bado ni mtihani Tanzania:Dkt.Bisimba

29 Novemba 2018

Utekelezaji wa tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa ni moja ya wajibu mkubwa wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa walioridhia tamko hilo la mwaka 1948. 

Hata hivyo kwa mataifa mengi licha ya kuweka katika katiba zake vipengele vya tamko hilo , utekelezaji unaostahili ndio umekuwa mtihani mkubwa. Tanzania kama ilivyo mataifa mengi yanayoendelea Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kuna baadhi ya vipengele vya tamko hilo imepiga hatua kubwa lakini kwingine inajikongoja. Tukimulika ibara ya 21 ya tamko hilo isemamayo “kila mtu ana haki ya kushiriki kwenye serikali yake, haki sawa ya huduma za jamii na serikali kutekeleza uongozi wake kwa kuzingatia matakwa ya wananchi.” Je Tanzania imefanikiwa utekelezaji wake ama la , tunapata ufafanuzi kutoka kwa mwanaharakati wa miaka mingi wa haki za binadamu nchini Tanzania Dkt. Helen Kijo Bisima.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter