Haki ya kuishi ni ibara ya tatu katika tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa. Ibara hii inasema kuwa kila mtu ana haki ya kuishi na kwamba haki hiyo inalindwa na sheria na hakuna anayepaswa kunyimwa haki hiyo.
Ibara ya 3
Kunyimwa kwa haki hii kunaweza tokea pale mtu anahukumiwa kifo kwani kuna baadhi ya nchi ambazo hazijatokomeza hukumu ya kifo.
Kumekuwa na msukumo kutoka Umoja wa Mataifa na pia kutoka kwa wanaharakati kwa nchi kutokomeza hukumu hii kwani inakiuka haki msingi ya binadamu.
Kenya ni moja ya nchi ambazo zimeondoa hukumu ya kifo lakini hali haikuwa hivyo awali na ndipo sasa Peter Ouko aliwahi kujikuta jela huku akiwa amehukumiwa adhabu ya kifo. Sasa anasimulia yaliyomsibu na harakati zake za kuondoa hukumu hiyo ambayo anasema sio muarubaini wa kuondokana na uhalifu.