Kila mtu ana haki ya kufurahia utulivu wa kijamii na kimataifa

Disemba 10, dunia itaadhimisha miaka sabini tangu kuridhiwa kwa tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa. Nyaraka hii imetajwa kuwa ya kipekee kwani imezingatia haki zote na imejumuisha makundi ya watu wote katika jamii ikiwemo makundi ya watu walio wachache.
Tamko hilo lenye ibara 30 imegusa maeneo yote ya haki za wote na nchi nyingi zimechukua muongozo wake katika kutunga sheria za nchi zao.
Ibara ya 28 ya tamko hilo inasema kuwa kiila mtu ana haki ya kufurahia utulivu wa kijamii na kimataifa ambapo haki zote zizlizopo kwenye tamko la haki za binadamu zinaweza kufurahiwa.
Ibara hii inaelezea umuhimu wa kuweka mazingira yanayowezesha mtu kufurahia haki zote kama zilizoorodheshwa katika tamko la haki za binadamu.